Ujerumani haitopeleka wanajeshi wake Iraq
16 Novemba 2003Matangazo
BERLIN: Serikali ya Ujerumani imekanusha matamshi ya Mwanadiplomasia wa UU, Xavier Solana kwamba uko uwezekano kuwa Ujerumani itapeleka wanajeshi wake Iraq. Katika mazungumzo aliyokuwa nayo mjini Berlin pamoja na Bwana Solana, Kansela Gerhard Schröder alisisitiza tena msimamo wa serikali yake kuwa Ujerumani haina kabisa niya ya kupeleka wanajeshi wake Iraq, kwa mujibu wa msemaji wa serikali. Bwana Solana alisema katika mahojiano aliyokuwa nayo na gazeti moja kwamba japokuwa kwa sasa Ujerumani haitopeleka wanajeshi Iraq lakini uwezekano huo utakuweko hapo siku za usoni.