Ujerumani haiko tayari kuidhinisha vikwazo vya EU kwa Israel
30 Agosti 2025Matangazo
Halmshauri ya Umoja wa Ulaya ilipendekeza kusimamisha kwa muda ufadhili wa utafiti katika makampuni kadhaa ya Israel, baada ya Uchunguzi wa Halmashauri hiyo kuonesha kuwa hatua za Israel, katika Ukanda huo zinakiuka mkataba wake na EU, unaotaka pande zote mbili kuheshimu haki za binaadamu.
Wadephul amesema mikakati iliyowekwa na EU haina athari yoyote katika hatua za kisiasa za Israel na operesheni yake ya kijeshi Gaza.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumaniamesema kile inachokifanya kwa sasa ni kuzuwia baadhi ya silaha zake kuelekea Tel Aviv, akiamini hiyo ndio njia iliyomuhimu na inayohitajika.
Umoja wa Ulaya umegawika kuhusu hatua sahihi za kuchukua katika vita vya Gaza na hali inayozidi kuwa mbaya.