Ujerumani-China/Nuklea:
12 Desemba 2003Matangazo
Berlin: Serikali ya Ujerumani inaripotiwa kusema kwamba inataka kukamilisha mkataba wa ujenzi wa kiwanda cha kinuklea nchini China haraka iwezekanavyo. Gazeti la Financial Times Deutschland ,limeripoti juu ya kuweko kwa waakilishi wa serikali ya China mjini Berlin Jumatano, kuzungumzia masuala ya kukamilishwa mkataba huo. Wanasiasa wa Ujerumani wengi wakiwa kutoka chama cha Kijani mshirika katika serikali ya Kansela Schröder, wamekosoa hatua hiyo ya kiwanda kinachomilikiwa na kampuni ya Siemens karibu na mji wa Hanau, kuiuzia China utaalamu huo. Wanahofia kwamba nchi hiyo inaweza kuutumia kutengeneza silaha za kinuklea. Ama serikali ya China imedokeza kwamba itakua tayari kusaini makubaliano yatakayoliruhusu Shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki, kulikagua eneo hilo la kinuklea.