Ujerumani: China ina "jukumu muhimu la amani ya kimataifa"
19 Mei 2025
Serikali ya Ujerumani imesema, Chinaina "jukumu muhimu la amani ya kimataifa". Waziri wa Mambo ya Nje Johann Wadephul ameyasema hayo hii leo Jumatatu alipokuwa akijadili kuhusu vita vya Urusi dhidi ya Ukraine na mwenzake wa China, Wang Yi.
Wito huo umetolewa wakati wasiwasi unaongezeka katika nchi za Magharibi kuhusu uhusiano kati ya China na Urusi, ambao unazidi kuimarika tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake kamili nchini Ukraine mwaka 2022.
Baada ya mazungumzo hayo ya simu ya mara ya kwanza kati ya Wadephulna Wang, wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imesema vita vya Urusi nchini Ukraine vinaathiri maslahi ya msingi ya bara Ulaya.
Wiki iliyopita Kansela Friedrich Merz, katika hotuba yake kuu ya kwanza bungeni tangu aingie madarakani, alisema Ujerumani ina wasiwasi kuhusu uhusiano wa karibu kati ya Beijing na Moscow na itaishinikiza China kuhakikisha "inachangia katika kutatua vita nchini Ukraine".