Uingereza yamteua mwanamke wa kwanza kuongoza MI6
16 Juni 2025Matangazo
Serikali ya Uingereza imemteua mwanamke wa kwanza Blaise Metreweli, kuongoza shirika la ujasusi wa nje la MI6 huku waziri mkuu Keir Starmerakisema nchi hiyo inakabiliwa na vitisho vikubwa ambavyo havijawahi kushuhudiwa.
Metreweli, afisa wa ujasusi kitaaluma ambaye kwa sasa anahudumu kama mkurugenzi wa teknolojia katika shirika hilo, atakuwa mkuu wa 18 katika historia ya miaka 116 ya shirika hilo. Atachukua nafasi kutoka kwa Mkuu wa MI6 anayemaliza muda wake Richard Moore wakati wa msimu wa vuli.
Mtu anayeteuliwa kuongoza shirika hilo la MI6 hufahamika kifupi kama "C" na ndiye afisa pekee anayetajwa hadharani kama mwanachama wa shirika hilo akiripoti moja kwa moja kwa waziri wa mambo ya nje.