Uingereza na mataifa 24 ya Ulaya yataka vita kuisha Gaza
21 Julai 2025Matangazo
Katika taarifa ya pamoja, mataifa hayo yamehimiza pande husika pamoja na jamii ya kimataifa kuungana katika juhudi za pamoja za kumaliza vita hivyo kupitia usitishaji mara moja wa mapigano, usio na masharti na wa kudumu.
Zaidi ya watu 85 wauawa wakisubiri msaada Gaza
Wakati huo huo waziri mkuu wa Palestina Mohammad Mustafa, amesema Israel inaendelea kutumia njaa kama silaha ya vita .
Katika hatua nyingine, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNRWA, limesema leo kuwa linapokea ujumbe wa kukata tamaa kutokana na njaa kutoka kwa wafanyikazi wake wa Gaza, wakati eneo hilo la Palestina likikabiliwa na viwango vinavyoongezeka vya njaa.