Uingereza na EU kutia saini makubaliano ya uhusiano
19 Mei 2025Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anatazamiwa kutia saini makubaliano ya uhusiano wa karibu zaidi kati ya nchi yake na Umoja wa Ulaya katika mkutano wa kilele wa kihistoria leo siku ya Jumatatu, hatua hiyo itafungua ukurasa mpya baada ya Uingereza kujiondoa kwa kwenye umoja huo miaka mitano iliyopita marufu "BREXIT".
Wawakilishi wa Umoja wa Ulaya wamesema wamefikia makubaliano na Uingereza baada ya mazungumzo marefu yaliyomalizika usiku wa kuamkia leo ambapo walijadili juu ya maeneo muhimu ya ushirikiano.
Eneo mojawapo ni suala mwiba la haki za uvuvi. Nick Thomas ni mwakailishi wa Umoja wa Ulaya aliyeshiriki mazungumzo hayo amesema "malengo yenyewe kama ninavyosema, ambayo tumekuwa tukijiwekea, ni mpango wa jumla kwa maslahi ya wavuvi wetu, njia rahisi za kuyafikia masoko ya kuuza samaki wetu. Na la pili, ni namna ya kutunza bahari zetu. Hayo ndiyo malengo ambayo tumeyafuata wakati wote katika mazungumzo."
Tangu alipoingia madarakani Waziri Mkuu Kier Starmer amekuwa akipambana kuyarejesha mahusiano baina ya nchi yake na Umoja wa Ulaya.