Uhariri wa magezeti ya Ujerumani hii leo
10 Desemba 2003Matangazo
Gazeti la OFFENBACH POST, linapozingatia kuvunjika kwa serikali ya muungano katika mkoa mdogo wa kaskazini mwa Ujerumani wa Hamburg, linaandika: Kiongozi wa serikali hiyo, Olwe von Beust, amechukua hatua barabara ya kukomesha mchezo wenye sifa mbaya ya mwanasiasa mshirika wa serikali Roland Barnabas Schill. Heko kwa hatua yake, lakini kwanini akachelewa kuchukua hatua hii mapema zaidi? Uchaguzi mpya uliopangwa kufanyika karibuni mkoani humo ni njia muafaka, hata ikiwa washirika wa von Beust wasingevuka kiunzi kinachodaiwa cha asilimia tano, hali ambayo ingemshurutisha von Beust kukubali muundo wa serikali kati ya vyama vikuu, CDU na SPD, au atawajibika kuwakabidhi kwa singo upande wengine madaraka.
Gazeti la shuguli za biashara HANSDELSBLATT, kuhusu mada hii linatabiri: Uchaguzi mpya mwishoni mwa mwezi Feburuari mwakani, utakuwa wa kuvutia masilahi ya kisiasa kote katika Ujerumani, kwa sababu utakuwa mwanzo wa chaguzi nyingine 14 zitakazofanyika mwaka ujao. Endapo chama-tawala cha CDU kitathibitishwa tena madarakani, hapana shaka chama kikuu mwenzi wake cha SPD, kitakumbwa na hali ya kuzidi kudidimia sifa yake miongoni mwa wapigaji kura. Lakini ishara hiyo ingezusha hali nyingine kabisa, nayo ni kwamba, chama cha Bw.Schill kingesambaratika, chama cha FDP kingeshuka chini ya kiunzi cha asilimia tano, na chama kikuu cha CDU, kingeadhibiwa kwa sababu ya kushindwa kutatua swala la haki sawa miongoni mwa raia.
Gazeti la mji wa mashariki wa Ujerumani wa Gera, OST-THÜRINGER ZEITUNG, linanapotilia uzito mjadala wa mageuzi ya serikali katika tume ya upatanishi, linaandika: Mnamo siku chache zilizopita, mbinyo katika tume ya upatanishi ulizidi kubana. Waziri mkuu wa mkoa wa Bavaria Stoiber, amejitolea kwa hiari kutoa ishara ya kuleta masikilizano, kati ya serikali na upande wa upinzani. Kama hoja zake zitafanikiwa, za kufanyika mkutano wa kilele wa viongozi wa vyama vya kisiasa, basi itakuwa wazi kwa kila mtu, ni nani aliye na usemi mzito katika muungano wa vyama-ndugu vya upinzani vya CDU na CSU. Hiki kingekuwa kipimo cha hatima ya kisiasa.
Gazeti la mji wa kusini mwa Ujerumani wa Munich, ABEND-ZEITUNG, linazingatia mada hii kwa kuandika: Cha kushtusha ni namna wanasiasa wa hadhi ya juu wanavyolishugulikia wakati huu swala hili. Hadi hii leo, hakuna raia hata mmoja, anayejua kile kitakachomkabili kuanzia tarehe mosi januari mwakani, kama tutawajibika kuendelea kutozwa kodi kama kawaida, au tutakabiliwa ghafla na hali mpya kabisa. Hii ni hali inayozusha hasira na kutoaminiwa tena wanasiasa wanaoshikilia hatamu za serikali. Mvutano huu katika swala la mageuzi ya kupunguzwa kodi na kubuniwa nafasi mpya za ajira, unashuhudia jinsi wanasiasa wasivyojali kile raia wanachotaka.
Gazeti la kusini mwa Ujerumani, SÜDDEUTSCHE ZEITUNG, linakamilisha uchambuzi wetu wa leo kutoka magazeti ya Ujerumani, kwa kutupia jicho ugomvi uliozuka kuhusiana na wazo la kuunzwa kiwanda cha kusafisha madini ya Plutonium cha mji wa Hanao kusini mwa Ujerumani, kwa kuandika: Siasa za serikali na za upande wa upinzani, zinahitilafiana sana. Tuchukue mfano wa karibuni: Serikali ambayo inafunga kiwanda cha madini ya kinyukilia nchini mwake, kwa sababu ya hatari itokanayo nacho, na iliyo na mpango wa kikiuza katika nchi za nje, kwa hakika hiki ni kama kitendawili. Na upande wa upinzani unaodai kupunguzwa viwango vya kodi, lakini ulio na wasiwasi iwapo mpango huu wa serikali ungefanikiwa, unakumbwa na hali ya kutofahamu chochote tena.

Matangazo