Uhariri wa mageti ya Ujerumani hii leo:
1 Aprili 2004Matangazo
Mada muhimu kabisa inayotiliwa uzito na magazeti mengi ya Ujerumani hii leo, ni mkutano wa pili wa kimataifa unaomalizika hii leo mjini Berlin, unaojadili hasa juu ya michango zaidi ya misaada, ujenzi mpya na urejeshaji wa demokrasia nchini Afghanistan. Gazeti la kusini mwa Ujerumani STUTTGARTER ZEITUNG, kuhusu mada hii linaandika: Kama Afghanistan itabahatika kujikwamua na kurejea katika maisha ya kawaida, hayo hayategemei hasa matatizo ya kifedha, ijapokuwa pesa pia ni muhimu. Bali baada ya vita vilivyodumu zaidi ya miongo miwili, baada ya tatizo kubwa la wakimbizi, kuharibiwa kwa nchi na ukandamizaji wa kiditeta kuna tatizo lingine kubwa la ukosefu wa hisia za raia kuwa taifa moja. Licha ya makundi ya kikabila yanayoshikilia misimamo inayohitilafiana, pia kuna wale wanaojulikana kamna watemi wa kivita, wanaosababisha kugawika kwa taifa la Afghanistan. Hata wafadhili wanashindwa kubuni mikakati inayofaa katika kuwaleta pamoja waAfghan. Gazeti Lingine la kusini mwa Ujerumani HESSISCHE/ NIEDERSÄCHSICHE ALLGEMEINE, linatoa maoni kama hayo kwa kuandika: Yameshapatikana mafanikio kwa kiasi nchini Afghanistani, baada ya kutilimuliwa utawala wa Taliban: Ikumbukwe kwa mfano wakimbizi zaidi ya Milioni tatu, waliorejea masikani zao za jadi, mafanikio ya kutungwa katiba ya mpito ambayo pia inawanahakikishia haki sawa wanawake, shule nyingi zilikwishafunguliwa tena, isitoshe pia yalikwishapatikana mafanikio ya kuundwa mfumo wa kuaminika wa polisi na wanajeshi. FRANKFURTER ALLGEMEINE nalo linaongezea: Mamlaka ya serikali ya rais wa mpito Hamid Karsai, haijafikia hali ya kutawala kama inavyotakikana. Ndio maana pia ni kwa sababu gani uchaguzi wa rais na bunge umeakhirishwa hadi mwezi septemba, ambao ulikuwa ufanyike mwezi juni. Katika nchi yenye makabila mengi na yenye kufuata destri za tangu karne na karne, ni vigumu kuhakikishwa urari wa mamlaka, ambapo kila mmoja angehisi kutotendewa visivyo haki.
Kuhusu mada hii gazeti la kaskazini mwa Ujerumani OSTSEE-ZEITUNG, linaandika: Baada ya vita vya kiraia vya tangu miaka 22, sasa zinahisiwa athari zake. Afghanistani imegeuka ni mojawapo kati ya nchi zilizo maskini duniani. Inahitaji misaada ya dharura, ndio maana duru hii ya pili ya mkutano wa kimataifa kuhusu nchi hiyo mjini Berlin, ni muhimu sana. Afghanistan inakabiliwa na mamatizo tele, kuanzia yale ya harakati za kupiga vita kilimo na biashara ya kasumba, wakulima kuteseka na uhaba wa maji, na watemi wa vita kuwa na uwezo wa kugharamia ushawishi kwa neema yao. Wakati asilimia 90 ya unga wa opium dunian hutoka Afghanistan, basi nchi hii inakutikana ni kitisho kikubwa kimataifa. Ndio maana mkutano wa kimataifa wa Berlin, unatafuta njia nyingine ya busara ya kiuchumi pindi kukomesha hatimaye biashara hii ya kasumba.
Nalo gazeti la MANNHEIMER MORGEN, linachangia mada hii kwa kuandika: Afghanistan huzalisha thuluthi mbili za mimea ya kutengenezea unga wa opium duniani. Biashara ya kilimo hiki ni nono, kwani mkulima hupata kiasi ya dola 12 000 kutoka kila hekta moja, kulinganisha na kiasi ya dola 300 tu kutoka kilimo cha mpunga. Kilimo hiki ndicho kinachowawezesha watemi kugharamia vita vya kimkoa na majeshi yao ya kibinafsi, wakulima binafsi hupata hela chache za kuwatuliza.
Tunakamilishiwa uchambuzi wa leo kutoka magazeti ya Ujerumani na yale gazet la MÄRKISCHE ODERZEITUNG linaandika kuhusu mada hii: Kitu kimoja kisisahauliwe, nacho ni hali ya wasiwasi inayowakabili wanajeshi wa kuhifadhi amani wa kijerumani katika mikoa wa Hindukusch nchini Afghanistan. Siku hizi imedhihiri katika Kosovo kwamba, bila ya utauzi wa kisiasa hapawezi kupatikana amani. Oparesheni za majeshi ya kimataifa, haziwezi kuhakikisha amani ya kudumu. Wakati huo huo inabidi kufafanuliwa: Endapo majeshi ya kutunza amani ya kimataifa yangehamishwa na kurejeshwa makwao, iwe ni kutoka Afghanista au maeneo ya Balkan, makundi yanayopingana na kikabila nchini Afghanistan, yangeanza ghafla kufarakana upya, hapana shaka wakiongozwa na wenye kufuata itikadi kali. Nchi za magharibi zinakabiliwa na mgogoro mgumu kweli kutatulika.

Matangazo