Uhariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo
6 Januari 2004Matangazo
Chama-tawala cha Kansela cha Social-demokratik, SPD, kinataka kuyafanyia mageuzi yajulikanayo "Agenda 2010" kwa jitihada ya kuufanyia halikadhalika mageuzi mfumo wa elimu kwa jumla. Kwa sababu hii magazeti mengi ya Ujerumaji, yanajishugulisha leo kinaganaga na umuhimu wa kujengwa chuo kikuu maalum cha wanafunzi wenye uhodari wa juu kinachopendekezwa na serikali. Mada nyingine muhimu n ucambuzi wa hali nchini Georgia bada ya uchaguzi mkuu wa karibuni na hali katika Afghanistan baada ya kuafikiwa katiba mpya nchini humo. Gazeti la mashuhuri la kusini mwa Ujerumani, FRANKFURTER ALLGEMEINE, linakumbusha kwamba, ujenzi wa chuo kikuu maalum cha wanafunzi wenye uhodari maalum, kwa dhati na kwa matumizi ya pesa nyingi, unasikika kuwa rahisi zaidi, kuliko kunyanyuliwa na kuungwa mkono hali ya utafiti katika vyuo vikuu. Badala yake wizara ya elimu ya Ujerumani, ina mpango wa kupunguza msaada wa fedha kwa ajili hiyo, nia ambayo itazusha athari za uwezekano wa upanuzi wa vyuo vikuu. Ni kweli, Ujerumani inawahitaji wasomi wenye uhodari maalum wa kisayansi, lakini sio kwa njia ya kujenga chuo maalum cha wanafunzi wenye uhodari maalum wa kimataifa.
Nalo gazeti mashuhiri kimataifa,DIE WELT, kuhusu mada hii linaandika: Katibu mkuu wa chama cha SPD, Olaf Scholz, amedhubutu kuzungumzia juu ya chuo kikuu cha wanafunzi wasomi wenye uhodari maalum, amekwenda mbali hata kumpita waziri mhusika na elimu, ambaye ananata katika sheria inayohusika na vyuo vikuu. Kama chama cha SPD, kwa kweli kina mpango wa kujenga chuo hicho katika Ujerumani, basi mtu ataweza kuelewa ni kwa nini kwa kutupia jicho utayarifu wa kuifanya sekta ya elimu, ni sehemu ya mashindano, ambayo si kila mmoja anayepindukia mshindi.
Gazeti la NEUE WESTFÄLISCHE la mji wa kaskazini wa Bielefeld, linakumbusha: Mtu akitupia jicho hali nchini Marekani, ambayo kiongozi wa kundi la SPD katika bunge, Franz Münterfering, anachukua kama mfano wa kuiga, anaelewa kwamba, ujenzi wa chuo cha hadhi ya juu, unamaanisha malipo ya juu ya karo. Ni kwa mafanikio makubwa katika kuboresha hali katika vyuo vikuu kwa jumla tu, ambapo itayaumkinika kujenga mustakabali wa elimu katika Ujerumani.
Gazeti mashuhuri la jiji la Kolon, KÖLNISCHE RUNDSCHAU, linatoa maoni kama haya linapoandika: Pindukio la chama cha SPD la kutaka kujenga chuo kikuu maalum, haliwezi kushangiliwa, iwapo kwa sababu hii vyuo vingine vikuu, vitaumia. Cha mstari wa mbele kabisa, kinabidi kiwe ni kuboreshwa masharti ya elimu na kuhakikishwa walimu ya wenye kipaji, badala ya kujengwa mradi wa kujitukuzia tu sifa. Ujenzi wa chuo maalum kwa wanafunzi wenye uhodari maalum, na sio kwa wanafunzi kwa jumla, hii ni nia ambayo haikubaliki.
Licha ya mada hii, magazeti mengine ya Ujewrumani, yanaendelea kutupia jicho mabadiliko ya kisiasa katika jamhuri ya zamani ya kirusi ya Georgia. Gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani,FRANKFURTER RUNDSCHAU, linafanya uchambuzi wa matokeo ya uchaguzi wa karibuni nchini humo, kwa kuandika: Gerogia, ambayo zamani ilikuwa ni jamhuri tajiri kabisa katika enzi ya kirusi, sasa imegeuka ndiyo maskini kabisa. Kwa sababu hii serikali ya mshindi wa uchaguzi huo Saakaschiwili, inakabiliwa na jukumu muhimu, la kufufua maendeleo ya kiuchumi, lakini iwapo tu Jamhuri hiyo, itakuwa na ushirikiano wa karibu na serikali za Moscow na Washington. Sharti lingine muhimu ni kwamba, rais huyu mpya, atabidi pia kuchukua hatua kali, za kuwapiga vita walajirushwa, makundi ya wafanyao vitendo vya kihalifu, na kuwachukulia hatua matajiri wakubwa wa zamani. Harakati hizi zimeanza kupamba moto tayari , mara tu baada ya ushindi wake.
Mada hii pia inazingatiwa na gazeti la mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Chemnitz FREIE PRESSE, linapoandika: Umashuhuri wa Saakaschwili, hautokani tu na mashambulio yake dhidi ya mamlaka ya kifedha. Na kwa kuwa sasa ameshanyakua madaraka, mwanasheria huyu, aliyechukua masomo nchini Marekani, anawajibika kushuhudia kwamba, yeye pamoja na wajumbe wa serikali yake, wanafahamu barabara majukumu yao yanayowakabili.
Uhariri wa leo katika magazeti ya Ujerumani, unakamilishwa na gazeti la MÄRKISCHE ODER-ZEITUNG, linapoeleza wasiwasi kuhusu mabadiliko ya hali nchini Afghanistan, baada ya kuafikiwa mapatano ya katiba mpya, kwa kuuliza, je, huenda ikawa kwanza itakuwa ikitawala hali ya demokrasia na neema ya wananchi au la? Hapana, kama kila mmojawapo anavyofahamu, miongoni mwa wale wanaotukuza mustakabali wa Afghanistan. Itakuwa kama ni ndoto, endapo sasa itajaribiwa kujengwa mfumo wa utawala wa mseto wa makabi, kwa kuiga msingi wa mtindo wa kimagharibi.
Matangazo