Uhariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo
29 Januari 2004Matangazo
Ijapokuwa waziri-mkuu wa uingereza, Tony Blair, amebahatika kuokoka kashfa kuhusiana na mtaalamu wake wa silaha aliyejinyonga Kelly, magazeti mengi ya Ujerumani yanazingatia jinsi waziri wa ulinzi, Geoff Hoon, atakavyoshindwa kuokoka , kutokana na ripoti ya uchunguzi, iliyoandaliwa na Lord Brian Hutton. Gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani, FRANKFURTER ALLEGEMEINE; kuhusu mada hii linaandika: Ni kweli wizara hii ya ulinzi, haikuapa kutowasilisha jina la Kelly kwenye vyombo vya habari, lakini mwanasayansi huyo hakujulishwa kwamba, jina lake linajulikna sana hadharani. Kwa sababu hii Kelly ana sababu nzuri za kuhisi kuendeshewa mambo kombo na mwajiri wake. Hali hii huenda ikawa kashfa karibuni kwa waziri wa ulinzi Hoon.
Mada hii pia inahaririwa na gazeti la mashariki mwa Ujerumani LEIPZIGER VOLKSZEITUNG, linapoandika: Naam, hakimu Hutton, amemtangaza waziri mkuu Blair, kutokuwa na hatia ya mtaalamu wake wa silaha Kelly kujinyonga, lakini wizara ya ulinzi ya uingereza, iliyokuwa mwajiri wa Kelly, inathibitisha kuwa yeye ndiye chanzo cha hatima yake ya mauti.
Nalo gazeti La kaskazini mwa Ujerumani, BRAUNSCHWEIGER ZEITUNG, linatabiri yale ambayo huenda yakamkumba kiongozi wa serikali ya Uingereza Blair kwa kuandika: Umashuhuri wake katika ofisi ya Downing Street, unaanza kufifia. Kwa mwanasiasa, ambaye amejipatia sifa kubwa hadharani kama Blair, hali hii ni chungu kabisa katika kipindi chake cha kuwa madarakani kwa muda wa miaka saba.
Magezeti mengi ya Ujerumani, leo yanazingatia kwa masilahi makubwa duru za uchaguzi wa rais zinazotangulia nchini Marekani wakati huu. Gazeti la mji wa kusini mwa Ujerumani wa Munich, ABENDZEITUNG, kuhusu mada hii linasema: mchuano wa mwisho bado uko mbali. Lakini michuano inayofanyika miongoni mwa wagombea wa chama cha kidemokrasi nchini Marekani, kwa kweli inavutia sana. Jonny Kerry amefanikiwa kushinda katika duru ya pili, dhidi ya washindani wake Howard Dean na Wesley Clark. Lakini katika mikoa ya kusini, atabidi kuwashuhudia wademokrasi wenzake kwamba, mgombea kutoka New-England, hawezi kukielekeza chama katika upande wa kushoto, bali kuelekea Ikulu kwa kupitia mkondo wa katikati. Ni John F.Kennedy pekee aliyefanikiwa katika mkakati huu hadi sasa mwaka 1960.
Nalo gazeti la WIESBADENER KURIER, kuhusu mada hii linaandika: Naam, ushindi kwa John Kerry, lakini pia ushindi kwa chama cha kidemokrasi. Haya ndiyo matokeo ya duru ya awali ya uchaguzi katika mkoa wa New Hampshire, ambayo karibu yalimtumbukiza mashakani mpinzani mkali dhidi ya rais Bush Howard Dean katika duru ya mkoa wa Iowa. Wademokrasi wanamtafuta mgombea mwenye kuzingatia mkondo wa wastani, ambaye pia ana uwezo wa kushindana dhidi ya rais Bush.
Mada nyingine inayotiliwa uzito na magazeti mengi ya Ujerumani, ni ile plani inayoendelea kujadiliwa, ya kudaiwa malipo ya malori yanayosafirisha shehena katika barabara kuu za Ujerumani. Gazeti mashuhuri kibiashara, HANDELSBLATT, kuhusu mada hii linaandika: Kwa sababu serikali bado haijapitisha uamuzi kamili, waziri wa usafirishaji hana njia nyingine ya busara, ataendelea kushikilia mkondo huo wa kudai malipo ya malori, ijapokuwa mjadala unaohusika, bado unaendelea. Wakati umeshawadia kwamba, viongozi wa makampuni mashuhuri ya Daimler na Telekom, Jürgen Schrepp na Kai-Uwe Ricke, wakumbushwe jukumu lao la kumkabidhi swala hili la usafirishaji wa malori kansela binafsi.
Gazeti la mashariki mwa Ujerumani DRESDENER NEUSTEN NACHRICHTEN, linatukamilishia uchambuzi wa magazeti ya Ujerumani hii leo, kwa kuandika kuhusu mada hii: Utahitajika muda wa miezi 16 hadi kukamilisha plani hii, wakati ambao utazusha hasara ya mabilioni ya pesa. Hii ni hali isiyo ya kawaida ya kufanyika makosa katika maswsala ya uchumi na siasa. Na kwa mara nyingine, mlipaji kodi ndiye atakayebebeshwa mzigo huu, kwa sababu mpango huo wa usafirishaji wa malori, hauwezi kutekelezeka kwa kiwango kilichokuwa kimetengwa hadi sasa.

Matangazo