Ujerumani: Ukweli, uzushi na chuki juu ya uhalifu wa kigeni
8 Aprili 2025Idadi ya makosa ya jinai yalioripotiwa ilipungua kwa asilimia 1.7 ambapo jumla ya matukio milioni 5.84 yalisajiliwa polisi. Lakini Hata hivyo kwa jicho la kichunguzi matukio haya yanatia wasiwasi mkubwa kama kweli hali ya usalama imeboreka kama jinsi inavyoonekana.
Waziri wa Mambo ya Ndani Nancy Faeser, na Mkuu wa Idara ya Polisi inayosimamia Makosa ya Jinai nchini Ujerumani (BKA), Holger Münch, wamesema miongoni mwa sababu zilizochangia kupungua kwa uhalifu ni hatua ya serikali ya kuhalalisha kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi binafsi.
Lakini viongozi hao bado wanapata wasiwasi kutokana na ongezeko la asilimia 1.5 la matukio ya vurugu yaliyopundukia hadi matukio 217,000, yakijumuisha mashambulizi ya kisu 18,000 .
Soma pia:Mmoja ashikiliwa kwa kumchoma kisu mtalii, mjini Berlin
Matukio haya yamezusha mijadala ya kisiasa nchini Ujerumani kila yanapotokea na mara nyingi washukiwa ni watu ambao sio raia wa Ujerumani. Katika hatua hii, mara nyingi huibua nadharia kwamba kuongezeka kwa wahamiaji ndio sababu ya kuongezeka uhalifu.
Mjadala wa uhalifu usioegemea chuki
Katika takwimu inashangaza kwamba idadi jumla ya washukiwa wote ambao matukio yao yamesajiliwa katika idara ya polisi, wengi zaidi ni wahamiaji ikilinganishwa na Wajerumani wenyewe, takwimu hizi zinaakisi matukio kama vile mauaji, ubakaji na hata matukio ya kwenye jamii kama vile unyang'anyi pamoja na ulanguzi wa dawa za kulenya.
Katika mukhtadha huu Mkuu wa Ofisi ya Makosa ya Jinai Ujerumani BKA Münch anasema aina hii ya uhalifu na uchunguzi wake hauegemei tu kwenye swala zima la "asili ya mtu" bali pia mkusanyiko wa matukio kadhaa ya hatari.
Ananonya kwamba hali ya ugumu wa maisha kwa wakimbizi ambao wanaishi katika kambi na hawaruhusiwi kufanyakazi, kwa mtazamo wake haya yote ni miongoni mwa sababu kuu ya kuongezeka kwa uhalifu miononi mwa wageni.
"Kuna msongo wa mawazo. Matukio ya kikatili ambayo hutokea mara kwa mara miongoni mwa wahamiaji hasa wakati wa utoto wao. Na mitazamo ya ukatili ni kawaida miongoni mwao."
Soma pia:Watu wawili wajeruhiwa katika shambulizi la kisu Berlin
Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Ndani Ujerumani Nancy Feaser anafahamu kwa undani namna ambavyo mjadala juu ya "uhalifu na uhamiaji" unavyoibua hisia na migawanyiko miongoni mwa watu nchini Ujerumani mara zote.
"Tunapoaswa kuzungumza hili bila kuchochea chuki, tunapaswa kuzungumza bila kusita. Lakini nasisitiza bila kuamsha chuki"
Katika mukhtadha huu alitaja pia kuhusu hali inayowakumba wakimbizi wengi ambao wanapewa mtazamo tofauti kabisa kuhusu Ujerumani na kile alichokiita magenge ya walanguzi.
Waziri huyo wa Mambo ya Ndani Ujerumani ametoa mtazamo wake kwa vyombo vya habari na kuvitaka kuripoti mara kwa mara juu ya ukweli kwamba wanapaswa kusalia kwenye kambi za wakimbizi huku kuunganisha ushauri huu na matumaini kwamba ari ya wageni kuelekea Ujerumani inaweza kupungua.
"Uhalifu wa kigeni" ni neno linalopotosha
Katika mtazamo wa kisayansi imethibitika kwa muda mrefu kwamba neno "uhalifu wa kigeni" linaweza kupotosha na linaweza kuchochea chuki.
Mtafiti Susann Prätor wa Chuo cha Polisi cha Lower Saxony, kwa miaka mingi amekuwa akifanya utafiti kuhusu uhamiaji na dhana ya uhalifu.
Alithibitisha katika matokeo ya utafiti wake kwamba suala la uhalifu halihusiani na asili ya mtu ama utaifa wa mtu bali ni hali ya kimaisha anayoishi mtu Ujerumani.
Soma pia:Muungano wa upinzani wa Ujerumani wajadili tena uhamiaji na masuala ya usalama
Prätor ambaye ni mwanasosholojia, mwanasaikolojia, na msomi wa sheria anabainisha kwamba miongoni mwa vyanzo vya uhalifu ni pamoja na umaskini, elimu ya chini, hali mbaya ya kifedha, kuishi katika hali mbaya na ukatili ndani ya familia
"Taswira fulani ya uanaume inaonekana zaidi katika makundi fulani ya wale wasio Wajerumani."
Mtaalam huyo pia anaeleza kwamba waathiriwa na mashahidi wengi huwaripoti zaidi wageni kuliko Wajerumani.
"Tafiti zimeonyesha kuwa watu wanaochukuliwa kuwa wageni wana uwezekano mkubwa wa kuripotiwa kuliko watu wanaochukuliwa kuwa Wajerumani." Aliongeza kwamba hiyo ni kutokana na muonekano ama namna wanavyozungumza.
Si wageni wote wanaofanya vitendo vya uhalifu
Mtaalamu Prätor kadhalika anaona ipo changamoto kwenye jamii ya kuwajumuisha pamoja wageni linapokuja suala la uhalifu.
Ameweka wazi kwamba wahamiaji kutoka Marekani, wakimbizi wa kivita kutoka nchini Syria, Waturuki waliokuja Ujerumani miongo kadhaa iliyopita, watalii na hata wale wanaoingia Ujerumani na kufanya uhalifu na kuondoka tena na wote wanalinganishwa na wale wenye uraia wa Ujerumani.
Katika kuweka usawia wa dhana hii potofu, katika takwimu za uhalifu ambazo hutolewa kila mwaka sasa zinawasilishwa kwa njia tofauti kabisa.
Soma pia:Ujerumani kuongeza kasi ya kuwarudisha wahamiaji makwao
Hii ikijumuisha idadi kubwa ya wanaume na vijana ambao si raia wa Ujerumani ni kubwa zaidi-- hili pia linaongeza viwango vya uhalifu.
Kwa sababu vijana na wanaume - bila kujali asili yao - wana uwezekano mkubwa wa kufanya uhalifu. BKA pia inaonyesha kwamba kuna uhalifu ambao unaweza tu kufanywa na wageni. Juu ya yote, ukiukwaji wa sheria za hifadhi na makazi.
Hatua hii ni kwa sababu vijana na wanaume bila kujali asili zao ni rahisi zaidi kutekeleza uhalifu, Ofisi ya Polisi ya Makosa ya Jinai Ujerumani imesema kuwa kuna matukio ya uhalifu pia yanafanywa na wageni. Juu ya yote kuna ukiukwaji wa sheria za hifadhi na makazi.