Uganda yawinda nusu fainali kwa kumenyana na Senegal
23 Agosti 2025Uganda Cranes wanaingia katika mechi hiyo wakiwa na matumaini makubwa baada ya kuongoza Kundi C na kutinga hatua ya mtoano ya CHAN kwa mara ya kwanza katika historia yao.
Uganda wanatarajiwa kupewa msukumo na mashabiki wa nyumbani katika dimba la Mandela mjini Kampala. Uganda inalenga kuwa mwenyeji pekee atakayebaki mashindanoni baada ya wenyeji wenza Kenya na Tanzania kuyaaga hapo jana.
Magadascar na Morocco zilitinga nusu fainali jana.
Uganda yatinga robo fainali ya kwanza michuano ya CHAN
Baadae leo usiku katika uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar, Sudan na Algeria zitakabiliana kutafuta tiketi ya mwisho ya nusu fainali.
Timu hizi mbili zinakutana kwa mara ya tatu katika historia ya mashindano ya CHAN.
Zilikutana mara ya mwisho mwaka wa 2011, na kutoka sare tasa katika hatua ya makundi kabla ya Sudan kushinda 1 - 0 katika mechi ya kumtafuta mshindi wa nafasi ya tatu.