Uganda yatinga robo fainali ya kwanza michuano ya CHAN
19 Agosti 2025Matangazo
Timu ya Uganda ililazimisha sare tasa ya mabao 3-3 mbele ya timu ya soka ya Afrika Kusini, matokeo yaliyoisafishia njia kufuzu robo fainali yao ya kwanza ya michuano ya CHAN.
Mchezo huo ulikuwa wa kufa na kupona kwa Uganda ambayo kwa pamoja na Tanzania na Kenya ndiyo zimeandaa michuano hiyo ya CHAN mwaka huu.
Afrika Kusini iliutawala mchezo hadi dakika za majeruhi ikiongoza kwa mabao 3-1. Hata hivyo vijana wa Uganda, the Cranes, walimudu kusawazisha mabao mawili mnamo dakika ya 88 na jingine ndani ya dakika 6 za nyongeza.
Kwa matokeo hayo Uganda iliibuka kinara wa kundi C na kusonga mbele robo fainali. Hapo jana Algeria nayo ilimudu kusonga robo fainali baada ya kulazimisha sare ya bila kufunguka na timu ya soka ya Niger.