SiasaUganda
Uganda yakubali kuwapokea waliokosa hifadhi Marekani
21 Agosti 2025Matangazo
Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda, Vincent Bagiire Waiswa, amesema katika taarifa kuwa makubaliano hayo ni ya muda na yenye masharti, ikiwemo kutowachukua watu wenye rekodi za uhalifu na watoto wasiokuwa na mlezi.
Waiswa ameongeza kwamba Uganda ingependelea kuwapokea watu wenye uraia wa Kiafrika chini ya makubaliano hayo.
Rais wa Marekani, Donald Trump analenga kuwafukuza mamilioni ya wahamiaji wanaoishi nchini humo bila vibali halali, huku serikali yake ikilenga kuwapeleka wahamiaji hao katika nchi ya tatu, ikiwemo kuwapeleka wahalifu waliokwishahukumiwa nchini Sudan Kusini na Eswatini.