Sheria na HakiAfrika
Uganda: Besigye afikishwa katika mahakama ya kiraia
19 Februari 2025Matangazo
Besigye ambaye alionekana kudhoofika na ambaye amekuwa kizuizini tangu mwezi Novemba, alirudishwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali mjini Kampala.
Kuendelea kuzuiliwa kwa Besigye kunavutia maoni zaidi huku wafuasi wake , wanaharakati pamoja na watu wengine wakionya kwamba anahitaji huduma ya matibabu na anapaswa kutolewa kutoka gerezani.
Soma pia:Jumuiya ya Madola yaihimiza Uganda kumuwachia Besigye
Wameongeza kuwa madhara yoyote kwake akiwa kizuizini yanaweza kusababisha machafuko mabaya nchini humo.
Familia yake inasema ameanza mgomo wa kula kulalamikia kuendelea kuzuiliwa kwake baada ya mahakama ya juu ya Uganda kutoa uamuzi mwezi uliopita kuwa mahakama ya kijeshi haiwezi kuwahukumu raia.