Ufilipino yapongeza kuondolewa kwenye orodha ya FATF
22 Februari 2025Baada ya kura wakati wa kikao chake cha kila mwaka, Shirika la kimataifa la kupambana na utakatishaji fedha la Financial Action Task Force - FATF lenye makao yake mjini Paris Ufaransa, liliiondoa Ufilipino kutoka kwenye orodha yake ya ufuatiliaji kufuatia mafanikio ya nchi hiyo na kusasisha taarifa zake kuhusu maeneo hatari yanayofuatiliwa.
Nchi kadhaa zaorodheshwa kumulikwa kwa utakatishaji wa fedha
Katika taarifa Jumamosi, Baraza la Kupambana na Utakatishaji Fedha mjini Manila, lilipongeza uamuzi huo wa FATF na kuutaja kuwa hatua muhimu ambayo italeta faida nyingi.
Hatua ya FATF itatoa afueni kwa mamilioni ya Wafilipino
Baraza hilo limeongeza kuwa hatua hiyo pia itatoa afueni kwa zaidi ya Wafilipino milioni mbili wanaofanya kazi nje ya nchi na kutuma pesa nyumbani kila mwaka. Ufilipino imekuwa katika orodha hiyo ya FATF tangu mwaka 2021.