Ufaransa yautaka Umoja wa Ulaya kuishinikiza Israel
29 Julai 2025Matangazo
Jean-Noel Barrot, waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, amewaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kwamba Kamisheni ya Ulaya, kwa niaba ya Umoja wa Ulaya, lazima ielezee waziwazi matarajio yake na ioneshe njia zinazoweza kutumika kuilazimisha serikali ya Israel kuyasikia matarajio hayo.
Barrot alikuwa akizungumza kwenye siku ya kwanza mkutano juu ya suluhisho la madola mawili ya Palestina na Israel, ambao unaendeshwa kwa pamoja kati ya nchi yake na Saudi Arabia.