Ufaransa yasema Iran ifikie suluhu ya nyuklia haraka
22 Agosti 2025Taarifa hiyo imekuja baada ya mazungumzo ya simu kati yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, wakishirikiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Lammy, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Johann Wadephul, na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas.
Wadephul amesema Iran haina budi kushiriki kikamilifu katika mazungumzo hayo ili kuepuka kurejeshewa vikwazo. Mazungumzo mengine yamepangwa kufanyika mwishoni mwa wiki ijayo.
Iran itaendelea kufanya mazungumzo na Shirika la Kudhibiti Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa
Awali, wanadiplomasia hao wa Ulaya walitishia kuirejeshea Iran vikwazo vya Umoja wa Mataifa iwapo Jamhuri hiyo ya Kiislamu haitarejea kwenye meza ya mazungumzo kuhusu mpango wake wa nyuklia.
Ulaya na Marekani wanadai kuwa Iran inautumia mpango huo kutengeneza silaha za nyuklia, madai ambayo Tehran imekuwa ikikanusha vikali.