Ufaransa yakabidhi kambi zake za mwisho nchini Senegal
18 Julai 2025Matangazo
Ufaransa imezikabidhi kambi zake mbili za mwisho za kijeshi nchini Senegal, na hivyo kuliwacha jeshi la Ufaransa bila kambi yoyote ya kudumu katika maneo ya magharibi na katikati mwa Afrika.
Mkoloni huyo wa zamani wa Senegal, Ufaransa, imekabidhi kambi ya Geille, ambayo ndiyo kubwa kabisa Afrika Magharibi, na kambi yake ya jeshi katika uwanja wa ndege wa Dakar, katika hafla iliyohudhuriwa na maafisa wa Ufaransa na Senegal.
Wanajeshi kiasi 350, waliokuwa na kibarua cha kufanya operesheni za pamoja na jeshi la Senegal sasa wanaondoka, kuashiria mwisho wa mchakato wa miezi mitatu wa kuondoka ulioanza mnamo mwezi Machi.