Urusi yatuhumiwa shambulio la mtandaoni dhidi ya Ufaransa
30 Aprili 2025Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot aliwasilisha shutuma hizo hapo jana kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, akiitaka Urusi kusitisha mara moja mashambulizi hayo.
Barrot amesema Urusi ilitumia aina ya programu ya ujasusi wa kijeshi unalojulikana kama "Fancy Bear", na ambao umehusishwa na mashambulizi ya mtandaoni kimataifa na kwamba Urusi imekuwa ikilenga sekta ya ulinzi, fedha na uchumi na kwamba mashambulizi hayo yanahusishwa na msaada wa Ufaransa kwa Ukraine kufuatia uvamizi wa Urusi.