Ufaransa: Urusi inafanya 'operesheni ya kujipigia debe'
22 Aprili 2025Barrot, ameliambia shirika la utangazaji la FranceInfo kwamba usitishaji huo wa mapigano katika kipindi cha Pasaka uliotangazwa ghafla, unalenga kuzuia kumkasirisha Rais Trump.
Urusi yapuuza sheria ya kudhibiti silaha
Barrot amesema hayo siku moja baada ya Urusi kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya Ukraine, hatua iliyokatiza ghafla makubaliano hayo dhaifu ya kusitisha mapigano.
Russia yafanya mashambulizi ya "kinyama" ya Krismas, Ukraine yasema
Trump ametishia kuachana na juhudi za kutafuta amani katika vita hivyo vya Urusi na Ukraine ambavyo vimedumu kwa miaka mitatu sasa, ikiwa hakutakuwa na hatua za maendeleo.
Wawakilishikutoka Marekani, Ukraine, Uingereza na Ufaransa wanatarajiwa kukutana mjini London wiki hii ili kuanza tena mazungumzo ya kusitisha mapigano nchini Ukraine.