MigogoroMashariki ya Kati
Nchi 3 za Ulaya zalaani "vitisho" dhidi ya Mkuu wa IAEA
30 Juni 2025Matangazo
Hayo ni baada ya Tehran kutupilia mbali ombi lake la kutembelea vituo vya nyuklia vilivyoripuliwa na Israel na Marekani.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran Esmaeil Baghaei amesema hivi leo kwamba haiwezi kutarajiwa kuhakikisha ushirikiano wa kawaida na IAEA wakati usalama wa wakaguzi wa shirika hilo hauwezi kuhakikishwa.
Iran imesema si tishio kwa mkuu huyo wa IAEA lakini inamtuhumu Grossi kwa kuchochea mashambulizi ya kwanza ya Israel kufuatia taarifa zinazokinzana alizozitoa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akitaja kuwa Iran ilikuwa ikikaribia kuwa na idadi ya kutosha ya madini yaliyorutubishwa lakini haikuwa na nia ya kutengeneza silaha za nyuklia.