Ufaransa na Ujerumani zaahidi kushirikiana katika ulinzi
7 Mei 2025Haya yanajiri wakati Ulaya inaazimia kuimarisha ulinzi wake hasa kutokana na vita vya Urusi dhidi ya Ukraine na mashaka juu ya ahadi za usalama za Marekani kwa Ulaya chini ya Rais Donald Trump.
Wakizungumza na katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Macron amesema, "Mwamko huu wa kimkakati kwa ulinzi wa Ulaya, tumekuwa tukiongeza kasi tangu Baraza la Ulaya mwezi Machi, na kwa pamoja, tutalazimika kufanya mpango uliopendekezwa na Tume ya Ulaya."
"Kuhamasisha ufadhili wa kibinafsi na wa umma kwa mahitaji ya uwezo wa kipaumbele, kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika msingi wetu wa ulinzi wa Ulaya wa viwanda na teknolojia."
Soma pia: Friedrich Merz aapishwa kuwa Kansela wa Ujerumani
Akizungumza kabla ya kuelekea Poland, Kansela Merz amesema kwa pamoja watachukua hatua ili kuimarisha zaidi uwezo wa kiusalama na ulinzi wa Ulaya.
Ufaransa na Uingereza zimekuwa zikiongoza majadiliano kati ya kile kinachoitwa "muungano wa walio tayari" wa nchi 30 kuhusu uwezekano wa kutumwa kwa wanajeshi ili kupata usitishaji vita vya Ukraine.