Ufaransa na Ujerumani walenga kusitisha tofauti zao
24 Julai 2025Matangazo
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Ujerumani Stefan Kornelius, Merz na Macron wamekubaliana kujaribu kusuluhisha tofauti zilizopo baina yao kuhusiana na mradi wa ndege za kivita wa FCAS unaohusisha Ujerumani, Ufaransa na Uhispania kufikia mwishoni mwa mwezi Agosti.
Mradi huo wenye thamani ya zaidi ya yuro bilioni 100 umechelewa kutekelezwa kutokana na malumbano pamoja na haki za umiliki za ndege hizo.
Mazungumzo ya viongozi hao yaligusia pia sera ya Ulaya, vita vya Ukraine na Mashariki ya Kati na mazungumzo ya kibiashara na Marekani. Hii ni baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia kuuwekea Umoja wa Ulaya ushuru wa asilimia 30 iwapo hakutofikiwa makubaliano ya kibiashara ifikiapo Agosti mosi.