Ufaransa kuitambua rasmi Palestina kama taifa huru
25 Julai 2025Macron amesema bado anaamini katika mustakabali wa suluhisho la serikali mbili ambayo amesema ndio njia pekee ya amani.
"Pamoja tunaelewa umuhimu wa uwepo wa muelekeo wa kisiasa. Ninaamini katika mustakabali wa suluhisho la serikali mbili kama msingi utakaotoa nafasi ya Israel kuishi kwa amani na usalama na majirani zake. Ninaamini katika tukiunganisha sauti mjini Paris london na mahali kwengine kutambua palestina kama dola na kuanzisha mchakato huu wa kisiasa ambao naamini ndio njia pekee ya amani," alisema Macron.
Ufaransa kuitambua rasmi Palestina kama taifa huru
Rais huyo wa Ufaransa ameongeza kuwa ni lazima vita visitishwe Gaza ili kuhakikisha ustawi wa raia pamoja na taifa la Palestina.
Uamuzi huo umeifanya Ufaransa kuwa taifa lenye ushawishi mkubwa zaidi barani Ulaya kuchukua hatua hiyo ya wazi, huku mvutano ukizidi kati ya Israel na Wapalestina.