Visiwani Comoro kuna kile kinachoitwa "harusi kubwa" au "ada" ama kwa kiingereza "the grand marriage." Ni utamaduni wa Wakomoro unaowafanya kutambulika kote duniani. Wanasema "ada" ni sawa na mauti, yaani ni lazima kila Mkomoro aipitie. Fahamu mengi zaidi katika "Utamaduni na Sanaa" na Saumu Mwasimba.
Wanaume wa Comoro wakiwa wamevalia mavazi rasmi ya sherehe ya adaPicha: Imago/imagebrokerZawadi za dhahabu anazotakiwa kutoa bwana harusi kwa bibi harusi katika sherehe ya ada Picha: Getty Images/AFP/I. YossoufWanawake Comoro wakicheza na kuimba katika sherehe ya adaPicha: Imago/imagebroker